TAA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 June 2022

TAA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 

Wahudumu wa ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), (kulia) wakimsikiliza Afisa Utawala wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Asia Shio (wa pili kushoto) akitoa maelezo mbalimbali wakati walipotembelea banda la maonesho la kiwanja hicho ikiwa ni Madhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16-23, Juni, 2022. Kushoto ni Afisa Uendeshaji, Albert Mutta na kulia ni Winfrida Osward, Afisa Usalama.

Meneja Masoko na Biashara wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Rose Commino (kushoto) akimweleza mjumbe wa zamani wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Dkt. Frederick Mwakibinga (kulia) masuala mbalimbali alipotembelea banda la maonesho la kituo hicho ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa (JNIA), Mhandisi Rehema Myeya (watatu kushoto) akiongea na wadau mbalimbali waliotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kituo cha JNIA ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma itakayofikia kilele tarehe 23 Juni, 2022.

Mmoja wa wamiliki wa maduka ya vitu mbalimbali yaliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Juzary Sayan akimsikiliza Afisa Uendeshaji wa kiwanja hicho, Albert Mutta wakati alipotembelea banda la maonesho la Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16-23, Juni, 2022. Katikati ni Afisa Utawala wa JNIA, Winfrida Duwe.

No comments:

Post a Comment