NYUMBA SACCOS YATOA MSAADA WA FIMBO NYEUPE 30 NA FEDHA KWA WASIOONA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 19 June 2022

NYUMBA SACCOS YATOA MSAADA WA FIMBO NYEUPE 30 NA FEDHA KWA WASIOONA

Viongozi wa Chama Cha Wasiona, Wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama na Viongozi wa Nyumba Saccos, nje ya ofisi za Chama hicho Sabasaba kwa mpili.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wasiona Khalidi N'gondo akipokea  fimbo nyeupe kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Nyumba Saccos Limited, Mwita Megabe wakati wa makabidhiano ya msaada huo.

Na Frida Manga

CHAMA Cha Wasioona Tanzania (TLB), Wilaya ya Temeke kimepokea fimbo nyeupe 30 na na fedha taslimu sh. lakimbli kutoka Chama cha kuweka na kukopa nyumba saccos Limited ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao za maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa chama hicho Protasi Mutakyanga alisema hitaji la chama hicho lilikuwa ni fimbo 285 ili kila mwanachama aweze kupata. Alisema baada ya kuona chama kina upungufu wa fimbo nyeupe walikiandikia barua nyumba saccos ili waweze kuwatatulia changamoto hiyo.

Mutakyangu alisema, licha ya chama chao kuwa na upungufu wa fimbo nyeupe pia bado wanachangamoto ya usafiri na mashine maalumu za kufanyia kazi zao.

“Tunaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidia ili nasisi tuweze kufanya kazi zetu kwa ufanisi mkubwa kwa ajili ya kujipatia maendeleo sisi wenyewe na Taifa letu,” alisema Mutakyangu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Khalidi N’gondo alisema hivi karibuni chama chao kitaadhimisha maadhimisho ya siku ya watu wasioona yatakayofanyika Mkoani Manyara .

Aidha Mjumbe wa Bodi ya Saccos Limited Mwita Megabe alisema, chama hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwainua wananchi mbalimbali.

Alisema kila mwaka saccos hiyo inavyofanya mahesabu inawakumbuka   watu wenye mahitaji muhimu kwa ajili ya kuwasaidia.

Alisema saccos yao mara nyingi hutoa misaada mblimbali kwa jamii lengo likiwa ni kuwakumbuka wahitaji.

Mnufaika mkuu wa wa saccos hiyo Ally Mbwana alisema saccos hiyo imemsaidia hadi kuwa na miradi kubwa.

Alisema hadi hvi sasa ameshakopa milioni 38 ambazo amezitumia kuchimba kisima cha maji safi na salama kwa ajili ya kuwasambazia wananchi wengine.


No comments:

Post a Comment