MWENYEKITI wa NURU FOUNDATION ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Zainab Kombo Shaib, amekutana na kufanya Mazungumzo na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Maryam Mwinyi.
Mama Zainab amefika katika Makaazi ya Rais Migombani Zanzibar, kwa lengo la kuitambulisha taasisi yake ya Nuru, na pia kujadili namna ya kufanikisha kwa mashirikiano, Dua Maalum ya Kuiombea Nchi, pamoja na Chakula cha Mchana kwaajili ya Watoto Yatima, Siku ya Eid ya Mfunguo Tatu.


No comments:
Post a Comment