KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Ujenzi), Balozi Mhandisi Aisha Amour, amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ya jiji la Dodoma na kiwanja cha ndege cha Msalato kuhakikisha wanazingatia viwango vya ubora katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza mara baada yakagua utekelezaji wa miradi hiyo jijini hapo, Balozi Aisha amesema kuwa kufanya hivyo kutawezeshamiradi hiyo kudumu kwa muda mrefu na kuweza kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
"Sisi kama Serikali tunataka kuona ubora wa kazi, miradi hii ikikamilika vizuri na kwa ubora itarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani na hivyo kuleta maendeleokwa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla", amesema Balozi Aisha.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amewataka makandarasi hao kuhakikisha kuwa wanatatua mapema changamoto zote zinazowakabili ili kuhakikisha miradi hiyo haikwami na inakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba.
Ameusisitiza Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) mkoani humo, kukagua na kufuatililia kwa karibu hatua kwa hatua
utekelezaji wa miradi hiyo ili kuona kuwa thamani ya fedha inayotumika
inaendana na mkataba.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa
wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda, amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa mradi huu
sehemu ya kwanza ya Nala- Veyula- Mtumba- Ihumwa Bandari Kavu ( Km 52.3)
umefikia asilimia 8.5 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2024.
Kwa upande wa Kiwanja cha ndege cha Msalato, Mhandisi Kabunda amesema kuwa hadi sasa Mkandarasi amekwishamaliza ujenzi wa kambi yake ya kuishi, karakana, boharipamojana mtambo wa kuzalisha kokoto na tofali.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Kiwanja hiki
unatarajiwa kujengwa kwa sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusisha ujenzi
wa miundombinu ambayo itajumuisha sehemu ya kurukia ndege, sehemu ya kupaki,
njia ya ndege, maegesho ya magari, uzio, mageti pamoja na barabara za
maingilio.

No comments:
Post a Comment