KATIBU MKUU UCHUKUZI AWATAKA TAA KUJIPANGA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 22 June 2022

KATIBU MKUU UCHUKUZI AWATAKA TAA KUJIPANGA

 

Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mathar Chidodo akimweleza Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire kuhusu miunodmbinu ya Kiwanja cha Bukoba, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua kiwanja hicho mkoani Kagera.

Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire (Kushoto) akiongea na wazee  wa Wilayani Misenyi, mkoani Kagera wakati alipokuwa katika ziara mkoani humo.

Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire akizungumza na Katibu tawala Mkoa wa Kagera  Profesa Faustin Kamuzora wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huyo alipommtembelea ofisini kwake Mkoani Kagera.

KATIBU Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha anaweka mpango mkakati wa ujenzi wa uzio imara wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba ili kuongeza usalama kiwanjani hapo. 

Ametoa kauli hiyo mjini Kagera mara baada ya kutembelea kiwanja hicho na kubaini changamoto ya uzio iliyotokana na changamoto za tabia nchi  na kuwataka kuzingatia kanuni na taratibu zinazoongoza usafiri wa anga. 


“Ni jukumu lako kama Meneja kuwasilisha changamoto hii Makao Makuu ili waje na mipango endelevu kwa changamoto hii sababu kwenye wizara hii tuna taasisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zungumzeni nao kupata ili kupata taarifa za nyuma ili kuweka mipango ambayo itanusuru miundombinu  hii’  amesema Katibu Mkuu Migire. 


Katibu Mkuu Migire amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya Viwanja vya ndege nchini ili kuwawezesha wasafirishaji kuamua njia wanayotaka kusafirisha mizigo, bidhaa na abiria na hatiimaye kuchochea maendeleo. 


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uwanja huo Matha Chidodo  amesema tabia nchi imekuwa ikiathiri miundombinu ya kiwanja hicho hususani uzio ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la maji katika Ziwa Viktoria. 


Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Migire amekagua miundombinu ya bandari ya Bukoba kuutaka uongozi wa Malaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha miundombinu hiyo inaboreshwa sambamba na ujio wa kukamilika kwa ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza. 

Naye Kaimu Meneja Bandari ya Bukoba amesema mradi wa upanuzi wa miundombinu uko katika bandari za Bukoba, Kemondo na Mwanza uko katika hatua za mwisho za manunzi na kumuhakikishia Katibu Mkuu kuwa kabla ya meli mpya kuanza kutoa huduma mradi utakuwa umekamilika. 

Katibu Mkuu Migire yupo Mkoani Kagera kukagua miundombinu na miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya Sekta hiyo.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment