Rais mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah. Picha na Maktaba. |
Na Adeladius Makwega - DODOMA
MEI 20, 2022 Wizara ya Habari na Tekinolojia ya Habari nchini ilisoma bajeti yake Bungeni, kwa bahati nzuri binafsi nilipata bahati ya kuisikiliza kwa karibu bajeti hiyo nikiwamo katika eneo jirani na bunge hilo na kwa sehemu nikiwa katika mkahawa wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sikupanga kuifuatilia bajeti hiyo lakini ilitokea tu kwa bahati, kwa hiyo nilichukua muda wangu mwingi kuisikiliza tangu mwenyekiti wa kikao hicho akiwatambulisha wageni wa wizara hii hadi waziri akiisoma.
Kwa nafasi yangu kama Mtanzania na mwanahabari nimebaini mapungufu saba ya bajeti hii lakini kwa heshima ya ndugu zangu watatu wanaofanya kazi wizara hapo ambao ni Primus Mungi, Jonas Kamaleki na Dkt Philip Filikunjombe mambo sita nitawakabidhi wao nikipata wasaa huo.
Ndugu Mungi, Kamaleki na Dkt Philikonjombe, hawa jamaa nawafahamu uwezo wao mkubwa wa uwanahabari wote watatu, la ziada kwa Dkt Filikunjombe ujuzi wake na umahiri wa sheria kwa miaka inayokaribia 20 sasa akiwa bingwa mambo ya sheria kwa kupata alama za juu ya masomo hayo tangu shahada yake ya kwanza ya sheria.
Ndiyo kusema mambo yangu sita ya kibindoni nitawaeleza naamini bajeti ijayo mambo yao yatakuwa mazuri sana.
Mwanakwetu hii ni wizara yetu bwana kwanini nikae kimya?
Lakini jambo moja naomba msomaji wangu nilisema kwa nia ya kuwa na vigezo vya utawala bora. Mwenyekiti wa kikao kile wakati anawatambulisha viongozi waliongozana na katibu mkuu wa wizara hiyo kumsindikiz waziri aliwatambua viongozi wa taasisi kadhaa za wizara hii miongoni mwao ni Bi Tuma Abdallah alitambulishwa kama Kaimu Mtendaji Mkuu wa TSN.
Alipotambulisha dada yangu huyu alisimama na kuketi, huku akivalia gauni ya rangi ya maziwa lenye madoa meusi. Swali ambalo liliibuka kwangu je mama huyu atakaimua uongozi wa TSN hadi lini?
Wakati mwenyekiti apomalizia utambulsiho huo alimualika Waziri wa Habari, alismama na kuanza kusoma bajeti yake. Nikiwa katika jengo la bunge nilizungumza na niliyekuwa naye jirani na kumuomba anielekeze uani ili nikachimbe dawa. Kweli niliekezwa huku Bajeti ikiendelea kusoma na mimi nilikuwa naisikiliza vizuri sauti ya waziri huyu.
Niliporudi katika eneo nililokuwa nimekaa, viongozi wa wizara hii waliotambulishwa wakiwa upande mwingine uliojaa sana walikuja kukaa nilipokuwapo mimi na nilimuona Dkt. Ayubu Ryoba naye alikaa kiti nilichukuwa nimekaa mimi. Kwa kuwa walingia wakubwa mie mdogo niliamua kutoka zangu kwa heshima zote nikamsalimia Dkt Ryoba kwa ishara na kuchukua begi langu na kutoka nje ya ukumbi huu.
Wakati ninatoka nikakutana ndugu Mungi akiendelea kuwaingiza viongozi wezake katika ukumbi huu japokuwa ulikuwa umeshajaa pomoni. Nilipokuwa natoka nikakutana na akina mama wawili nilipowatazama nikawaona kama mzao wangu tu. Wakaongea na mtu aliyekuwa mbele yangu kuelekezwa pahala fulani.
Wao mbele mie nyuma, nikabaini kuwa yule dada mmoja ni Tuma Abdallah wa TSN, nilimtazama kwaj icho la wizi, alafu nikamtazama kwa jicho pembe alafu mawazo yangu yakakumbuka ule utambulisho wa Mwenyekiti wa kikao cha Bunge.
“Tuma Abdalla ni Kaimu Mtendaji wa TSN.”
Nikasema huyu ndugu yangu wanamkaimisha nafasi hiyo tangu mtoto yupo darasa la nne hadi amaliza la saba bado anakaimu kwanini?
Haya niliyawaza kimoyo moyo tu, huku Tuma Abdallah mbele mie nyuma. Wakafikia katika mlango waliokuwa wanaenda, mimi nikatoka zangu katika viwanja vya Bunge.
Nikajiuliza hivi TSN ikipelekewa habari juu ya halmashauri fulani kuwa na wakuuu wa idara wanaokaimu kwa muda mrefu nafasi zao, je TSN wanaweza kuandika na kutoa habari hiyo katika magazeti yao?
Msomaji wangu jibu lake unalo.
Utaratibu wa kukaimua nafasi kw a utumishi wa umma ni miezi sita tu ikizdi mwaka mmoja hapo akimaliza anayekaimu anapewa barua yake, kinyume chake hilo linatazamwa kuwa siyo utawala bora.
Lakini je mbona jambo hili alizungumzwi? Wakati Jaji Mkuu wa sasa anakaimu nafasi hiyo wanasheria walisema sana na kulipigia kelele, je kwanini wanahabari wako kimya kwa jambo la ndugu yao? Je wanaweza kuisemea jamii yao kama kujisemea wenyewe wanshindwa?
Msomaji wangu jibu unalo.
Kama TSN na TBC wakiwa na watu imara serikali inaweza kuyapata mengi kupitia vyombo vyake vyenyewe na siyo kutumia mitandao ya kijamii na vyombo binafsi.
Binafsi ninaona kuwa kukaimu kwa Tuma Abdallah TSN inatosha sana anapaswa kukabidhiwa mikoba ya taasisi hiyo na jambo hili naliweka mezani kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga.
Nilipotoka katika viwanja vya bunge niliongea na mwanahabari mmoja, akisema kuwa Tuma Abdalla anauzoefu katika uandishi wa habari tangu akiwa binti mdogo sana sasa anakaribia miaka kati 25-28 kazini, alisikitika sana akasema kwa utani huyu anayekwamisha Tuma Abdalla itabidi tuchange pesa tukamloge kwa waganga.
Tulicheka sana, watu wanachange pesa wakamloge huyo mkwamishaji anayejijua yeye mwenyewe, kama wataenda Tanga au Bagamoyo hilo lipo katika imaya yao. Kwa kuwa mie sipende ulozi nawahi mapema kumshitakia mkwamishaji huyo kwa Balozi Katanga, huyu ni muugwana sana atalifanyia kazi jambo hili mapema sana.
Baada ya mjadala huo kila mmoja alichukua njia yake kurudi kwake.
NB Ifahamike wazi kuwa maoni haya yaliyo katika simulizi ni ya Adeladius Francis Fidelis Makwega wa Mbagala Sabasaba si maoni ya Tuma Abdalah.
0717649257
No comments:
Post a Comment