RC SENDIGA APIGA MARUFUKU KUPANDISHA BEI ZA BIDHAA HOLELA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 2 May 2022

RC SENDIGA APIGA MARUFUKU KUPANDISHA BEI ZA BIDHAA HOLELA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa katika ziara kuangalia ongezeko la bei kwa wafanyabiashara mkoani humo na kuongea na wafanyabiashara wa soko kuu kuhusiana na kupanda bei kwa bidhaa kama matunda,vyakula ,lakini baadhi ya wafanyabiashara kama  wauzaji wa mbolea wamesema mfumuko wa bei upo kawaida.

Na Fredy Mgunda, Iringa

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amepiga marufuku kwa wafanyabiashara kupandisha bei kiholela kwa ajili ya kupata faida hivyo wanatakiwa kupandisha bei kwa kufuata sheria za nchi ili kuondolea maumivu wananchi wa kawaida ambao ndio wanunuaji wa bidhaa hizo.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kuangalia bei ya bidhaa zilivyopanda mkoani Iringa, Bi. Sendiga alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wanatumia kigezo cha kupanda bei kwa mafuta nao ndio wanapandisha bei.

Sendiga alisema wafanyabiashara wakipandisha bei kiholela wanawaumiza wanunuzi na wananchi wa kipato cha nchi hivyo wanatakiwa kupandisha bei kwa kufuata sheria na tamko rasmi kutoka serikalini.

Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa alibaini kuwa vituo vyote vya mafuta ya petroli na dizeli vinauza mafuta hayo kwa kufuata sheria za nchi na muongozi ulitolewa na mamlaka husika hivyo aliwapongeza wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta.

Sendiga alisema kuwa wafanyabisha wengi wamepandisha bei kwenye vyakula, matunda na bidhaa nyingine ambazo zinazalishwa kwenye viwanda ambavyo vipo nje ya mkoa wa Iringa jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi kwa mamlaka nyingine zinazohusika.

Alisema kuwa ikibaini kuna mfanyabisha amepandisha bei kiholela atachukuliwa hatua kali za kisheria na hakutakuwa na msamaa kwa mfanyabiashara huyo.

Sendiga alizitaka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya kazi zao kwa weredi kwa kuwa wameoneka kuwa wameshindwa kudhibiti vipimo vya mizani pamoja na baadhi ya mabasi kupandisha bei nauli kinyume na sheria.

Kwa upande wa baadhi ya wafanyabishara wa mkoa wa Iringa walisema kuwa kupanda kwa bei ya mafuta ya magari kumesababisha kupanda kwa gharama za usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa za viwandani hivyo kusababisha nao kupandisha bei.

Walisema kuwa wanalazimika kupandisha bei za bidhaa mbalimbali ambapo inaonekana kama mzigo wote huo unamuangukia mtumiaji wa mwisho wa bidhaa hizo.

Aidha wafanyabiashara hao walimuomba mkuu wa mkoa wa Iringa kufikisha kilio chao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan juu ya mfumko wa bei ambao unaendelea maeneo yote nchini.

No comments:

Post a Comment