BENKI YA NMB YAZINDUWA RASMI KAMPENI YA TELEZA KIDIJITALI, DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 10 May 2022

BENKI YA NMB YAZINDUWA RASMI KAMPENI YA TELEZA KIDIJITALI, DAR ES SALAAM


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mpozi akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo mitaani kupata maoni yao kwenye uzinduzi wa kampeni ya NMB Teleza Kidijitali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mpozi akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo kupata maoni yao mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya NMB Teleza Kidijitali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mpozi wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Teleza Kidijitali iliyofanyika leo Tawi la NMB Tandika jijini Dar es Salaam.

BENKI ya NMB imezinduwa rasmi Kampeni ya Teleza Kidijitali, ambayo imelenga kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa kutumia na kunufaika na huduma zilizo chini ya kampeni hiyo za NMB Pesa Wakala, Lipa Mkononi na Mshiko Fasta.

Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam katika Tawi la Benki ya NMB Tandika, ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo waliwatembelea wafanyabiashara madukani mara baada ya tukio hilo kuwapa elimu zaidi. 

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mpozi akizungumza na baadhi ya waendesha bodaboda mitaani mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya NMB Teleza Kidijitali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakitoa huduma mitaani kwa wateja mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo.

 Akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi, Bi. Zaipuna alisema NMB imelenga kutoa elimu ya kutosha na kuwaingiza Watanzania wengi zaidi kwenye sekta rasmi ya kifedha ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa.

 “Tuko hapa kunadi huduma zote muhimu zilizopo kwenye mwamvuli wa Teleza Kidijitali, ikiwa ni ufunguaji wa akaunti za NMB, Mshiko Fasta ambapo mteja anaweza kupata mikopo nafuu isiyo na dhamana kupitia simu yake tu.”

 “Pia tumeutumia uzinduzi wa kampeni hii kwa ujumla kunadi huduma ya Lipa Mkononi, ambayo itamuwezesha mfanyabiashara kulipwa na wateja wake kwa kutumia lipa namba au kwa kuskani QR, huku ikitupa sisi kumbukumbu na historia ya mfanyabiashara huyo, kutusaidia hata katika utoaji wa mikopo. 

 “Pia tumekuja na NMB Pesa Wakala, huduma inayomuwezesha mtu yeyote kuwa wakala kwa kupitia simu yako ya mkononi (smart phone au tochi) kutoa huduma za kuweka, kutoa au kutuma pesa kirahisi,” alisema Zaipuna, ambaye alishiriki kutembelea wafanyabiashara wa eneo la Tandika madukani mwao kutoa elimu na kusikiliza maoni yao.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, aliwataka wakazi wa kanda yake kuchangamkia fursa zilizomo ndani ya kampeni hiyo, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bila kusumbuka kwenda matawini.

Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akisalimiana na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Benki ya NMB mara baada ya kuwasili Tawi la NMB Tandika kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Teleza Kidijitali jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB mara baada ya kuwasili Tawi la NMB Tandika kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Teleza Kidijitali jijini Dar es Salaam.

Huduma ikitolewa mitaani mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo.

Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (kulia) akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (kushoto) mara baada ya kuwasili Tawi la NMB Tandika kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Teleza Kidijitali jijini Dar es Salaam. Katikati ni fisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mpozi.


Wafanyakazi wa NMB wakijipanga kuwatembelea wateja na wananchi mtaani mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Teleza Kidijitali jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment