KINANA AWATAKA WABUNGE NA MADIWANI KUTOPITISHA SHERIA ZINAZOMINYA HAKI NA KUWABANA WANANCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 25 April 2022

KINANA AWATAKA WABUNGE NA MADIWANI KUTOPITISHA SHERIA ZINAZOMINYA HAKI NA KUWABANA WANANCHI

Makamu mwenyekiti wa ccm bara Comrade Abdulrahmana Kinana Akifurahia nyimbo ya Kikundi Cha ngoma ya Asili ya Watu wa Mwambao.

WANACHAMA NA VIONGOZI MBALIMBALI WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO.

Makamu Mwenyekiti ccm Bara comrade Abdulrahman Kinana kizungumza na mama mjasiriamali aliyekuwa akiuza bidhaa zake nje ya ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe ambako Kinana alifanya mkutano na wanachama na viongozi wa Chama hicho mkoa wa Tanga leo Jumatatu 25th April.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI/CCM MAKAO MAKUU).

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka  madiwani na wabunge kukataa  kupitisha  miswada ya Sheria  yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka  kulitazama vyema  kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.

"Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.

"Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano...sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane  na wananchi," alisema.

No comments:

Post a Comment