HAKIELIMU KUMSOMESHA 'BINTI KINARA' SEKONDARI YA VING’HAWE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 24 March 2022

HAKIELIMU KUMSOMESHA 'BINTI KINARA' SEKONDARI YA VING’HAWE

Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage akimpongeza mwanafunzi Mariam Malangusi aliyefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne Shule ya Sekondari ving’hawe (amepata daraja la kwanza alama 11). 

BINTI kinara kiongozi wa Championi aliyehitimu kidato cha nne mwaka 2021 na kupata daraja la kwanza la alama 11, daraja la kwanza pekee kwenye shule ya Sekondari ving’hawe, licha ya kupitia changamoto kubwa za maisha, amekuwa mfano mzuri kwa wasichana wengi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Binti huyo Mariam Malangusi kwa sasa aanasubiri kupangiwa shule ya kujiunga kidato cha tano huku ndoto zake zikiwa ni kusoma masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati amepata bahati ya kulipiwa gharama zote za ada atakapojiunga na kidato cha tano.

Hatua hiyo imetokana na kumgusa Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage ambao ndio wasisi wa vilabu za Vinara 'Champions' kwenye shule takribani 127 Tanzania bara, Alipotembelea shule aliyohitimu kidato cha nne na kupata ushuhuda toka kwa mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Daud Elias na kuamua kumtafuta ili kumpa moyo na kutoa ahadi hiyo.

Dkt. Kalage amesema HakiElimu katika mradi wa kusaidia wanafunzi wa kike kufanya vizuri kwenye sekta ya Elimu waliamua kuanzisha vilabu hivyo vya mabinti vinara ambao wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya wenzao na mwenendo wao kwenye masomo na changamoto nyingine.

“Sasa tumefurahi sana na nimefurahi siku ya leo nilipotembele shule ya Ving’hawe nikaambiwa shule imepata ‘Division one’ moja na aliyepata ni mmojawapo wa mabinti vinara, nikatamani sana nimuone nimpe pongezi zangu, na bahati nzuri ameletwa hapa, ni mfano mzuri kwa watoto wa kike kwamba wakipewa mazingira mazuri wanaweza, na changamoto zile zikiondoka wanaweza kufanya vizuri kuliko hata wavulana, mfano mzuri ni shule ile ambapo wasichana wanafanya vizuri kuliko wanaume, aliseme Dkt. Kalage.

Dkt. Kalage akaongeza kuwa.. “Sasa huyu binti nataka niahidi leo kwamba, Shirika la HakiElimu litamlipia ada yote ya miaka miwili atakayosoma 'A level' kwa kuwa mfano bora kwa watoto ambao wanafanya vizuri, najua 'A level' kuna school fees, kule chini Serikali imeondoa lakini kule juu unapaswa kulipa ada, tutawasiliana, na tutaangalia mambo mengine ambayo tunaweza kuyafanya kwako wewe ili iwe mfano kwa watoto wengine wa kike kwamba kumbe ukijitahidi kufanya vizuri unaweza ukaonekana na ukapata fursa nyingi zaidi. Alihitimisha Dkt. Kalage.

Mpaka sasa HakiElimu imeshirikiana na wananchi kukamilisha mradi wa choo cha kike cha kisasa chenye chumba maalumu kwa ajili ya kujisitiri wanafunzi wa kike, pamoja na mradi wa maji kwenye shule ya msingi Idilo ambao unalenga kuwasaidia zaidi watoto wa kike na wa kiume pamoja na wananchi wanaozungka shule hiyo, miradi yote imegharimu takriban Tsh Milioni 48 mpaka kukamilishwa kwake.

No comments:

Post a Comment