RAIS SAMIA AWAVUTA IKULU PROF. KABUDI NA LUKUVI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 10 January 2022

RAIS SAMIA AWAVUTA IKULU PROF. KABUDI NA LUKUVI

Profesa Palamagamba Kabudi.

RAIS wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassana amesema amewaacha makusudi katika baraza jipya la mawaziri Profesa Palamagamba Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi maana ana kazi maalum ya kuwapa Ikulu.

Rais Samia Hassana ameyasema hayo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma alipokuwa akiwaapisha mawaziri na manaibu mawaziri, makatibu na naibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali. Amefafanua kuwa amewapa kazi mpya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Lukuvi.

Rais Samia amesema; “Nataka niseme jambo moja tu nina kaka zangu, Lukuvi na Kabudi mko wapi? Kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu wanisaidie ili waje kunisimamia ninyi, kwa hiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo listi watakuja kwangu tuwasimamie ninyi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia alipongeza kazi nzuri aliofanya Kabudi kuhusu mazungumzo ya serikali na mashirika mbalimbali.

"Ila kazi yake kwa sababu haiko kwenye muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi ..mashirika yote kazi zote zitakazoingia ubi ana serikali, Kabudi ataongoza hiyo team."

Kuhusu Lukuvi rais alisema; "Kakangu Lukuvi yeye ana kazi na mimi.Mtaisikia baadaye lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi".

No comments:

Post a Comment