WIZARAYAKEMEA MAUAJI YA WANAWAKE MWANZA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 21 January 2022

WIZARAYAKEMEA MAUAJI YA WANAWAKE MWANZA...!

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, (Mb).

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi  Maalum imepokea kwa masikitiko mauaji ya Wanawake watatu yaliyotokea tarehe 19 Januari, 2022 na miili yao kuokotwa eneo la MECO Kusini, wilayani Ilemela, Mkoa wa Mwanza.

Kufuatia tukio hilo, Wizara inatoa pole kwa Ndugu na Jamaa, marafiki na wafiwa  wote walioguswa na msiba huo mzito.

Wakati vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo, Wizara inaendelea kukemea vikali vitendo vyote vya ukatili ikiwemo tukio hilo la mauaji.

Mungu awapumzishe marehemu wote. 

Imetolewa na;


Prudence Constantine

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


No comments:

Post a Comment