BARAZA LA WAZEE WA CCM WILAYA YA DODOMA MJINI WATEMBELEA UJENZI WA MJI WA SERIKALI, DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 23 January 2022

BARAZA LA WAZEE WA CCM WILAYA YA DODOMA MJINI WATEMBELEA UJENZI WA MJI WA SERIKALI, DODOMA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Dkt.Pindi Chana akizungumza na Baraza la wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma Mjini wakati walipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Pindi Chana akiwasikiliza wazee wa Baraza la wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma Mjini wakati walipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma  Mjini Meja Mstaafu Johnick Risasi akizungumza wakati wazee hao walipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma Mjini wakipata maelezo juu ya ujenzi wa miradi ya ukumbi wa mikutano na hoteli inayojengwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika eneo la mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Peter Mavunde akizungumza wakati wazee hao walipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mji wa Serikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.

Katibu wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma na Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bw Meshach Bandawe akieleza maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali kwa Baraza la wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma Mjini wakati walipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa mjihuouliopo Mtumba Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment