NA MWANDISHI WETU MAALUM MADRIDI, HISPANIA
TANZANIA yapongezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kwa namna ambavyo ilifanikisha kufanya Onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha lililokuwa na lengo la kutangza utalii katika nchi za Jumuiya za ukanda huo.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololkashvir wakati akitaja baadhi ya nchi za Afrika ambazo licha ya changamoto ya ugonjwa wa Korona lakini zimeendelea kufanya vizuri katika suala la utalii.
Ameyasema hayo mapema jana wakati alipokuwa akitaja baadhi ya mafanikio yake katika Uongozi wake tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UNWTO katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa 24 wa UNWTO ulipoanza.
Amesema Tanzania ni moja kati ya nchi katika bara la Afrika zinazochipukia katika kuhakikisha sekta ya utalii inafanya vizuri kwa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa ajili ya kutangaza vivutio vyake vya utalii.
Ametaja Onesho la kwanza la Utalii la Afrika Mashariki (EARTE) kuwa Tanzania imeonesha ukomavu na ujasiri wa hali ya juu katika kulifanya kwa mafanikio makubwa Onesho lile licha ya kuwa na muda mfupi wa maandalizi na uwepo wa changamoto a ugonjwa UVIKO -19.
'' Kati ya nchi za Afrika ninazoziona zinakwenda kuongoza kimapato kwa kuifanya sekta ya utalii kuwa namba moja huwezi kuiacha kuitaja Tanzania '' am so proud of you Tanzania'' alisema Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab
Akizingumzia pongezi hizo, Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab kwa kuonna na kukubali jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kufanya vizuri kimapato.
''Tumepongezwa kwa namna ambavyo tumeweza kufanya onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki. Sisi tuliona dogo, lakini wenzetu huku katika nyanja za kimataifa waliliona kubwa '' alisema Dkt. Ndumbaro.
Amesema Onesho la EARTE pamoja na mkutano huu wa UNWTO kwa nchi ya Tanzania ni fursa ya skuweza kutangaza utalii, lakini kama fursa ya kuwavuta wenzetu watalii waje pia nchini Tanzania katika kuwekeza kwenye sekta ya utalii.
Dkt. Ndumbaro amesema pongezi hizo zinatia moyo yta kuongeza kasi zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania '' Tumepongezwa na nimesema kwamba kumbe kweli watanzania wanaweza kufanya mikutano kwa kiwango kikubwa zaidi’’ alisema Dkt. Ndumbaro.
Kupitia Pongezi hizo, Dkt.Ndumbaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan kwa Ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwake huku akitaja Kampeni maalum cha kutangaza utalii wa kupitia kipindi cha ' Royal Tour' aliyoiasisi yeye mwenyewe kuwa hali inampa nguvu zaidi katika kutangza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro katika mkutano huo wa siku nne unaoendelea kufanyika katika Jiji la Madrid anatumia fursa hiyo ya kushiriki katika kuwaalika Viongozi mbalimbali wa Kidunia Mawaziri wa Utalii pamoj na Wataalamu mbalimbali wa utangazaji na masuala ya utalii katika kuwaalika kushiriki katika Mkuu wa Utalii wa Kanda ya Afrika ambapo Tanzania anataraji kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo utakafanyika Oktoba 6 hadi 8 mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment