Na Dotto Mwaibale, Hanang
VIFAA vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya Sh.100,000,000.00 (Milioni mia moja) vimechangishwa na makundi mbalimbali wilayani Hanang mkoani Manyara katika kilele cha wiki ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho kilichofanyika katika viwanja vya ofisi ya wilaya hiyo akizungumza na wananchi wakati akipokea vifaa hivyo alimpongeza mkuu wa wilaya hiyo Janeth Mayanja kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuhamasisha maendeleo wilayani humo.
Vifaa vilivyopokelewa katika kilele hicho ni mbao, mchanga, saruji, Gypsum board, Gypsum Powder,vigae, mbao, misumari rangi za aina mbalimbali ambavyo vinakwenda kutumika kukarabati miundombinu ya Hospitali ya Tumaini wilayani Hanang.
Katika maadhimisho hayo mgeni wa Heshima alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu Fredrick Tluway Sumaye.
Wiki hiyo ya maendeleo wilayani humo iliandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo Janeth Mayanja lengo likiwa kutatua kero mbalimbali wilayani humo hasa katika Hospital ya Wilaya ya Hanang.
Katika kuitikia mpango huo mzuri wa maendeleo uliobuniwa na mkuu wa wilaya hiyo wadau mbalimbali walijitokeza kuchangia ikiwemo wafugaji,wakulima,Taasisi za Dini,wafanyabiasha,wajasiriamali, makampuni,Taasisi mbalimbali klabu za mpira mkuu wa wilaya amewashukuru wananchi na wadau wote wa maendeleo kwa kuchangia kwa hiari vifaa hivyo ili kuunga jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu.
No comments:
Post a Comment