Kijana wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jijini Arusha, Nathan Kimaro amemzawadia nakala ya kitabu cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (MZEE RUKHSA), Msomi na Mwanajumui wa Afrika (Pan-Africanist) Profesa Patrick Lumumba hapo jana jijini humo. Prof Lumumba alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Taasisi ya WAJIBU, uliofanyika kwa siku mbili (Novemba 18-19,2021) jijini Arusha uliohusu masuala ya Uwazi, na Uwajibikaji kwa mwaka 2021 (International Transparency and Accountability Conference 2021 (ITAC 2021).
Siku ya Familia Duniani: Wito wa Kudhibiti Ongezeko la Watu Kuokoa Uchumi
wa Taifa
-
KATIKA maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani, wito umetolewa kwa familia
za Tanzania kuzingatia uzazi wa mpango kama njia muhimu ya kujenga familia
imara...
1 hour ago

No comments:
Post a Comment