BARABARA YA SAME - MKOMAZI KUJENGWA KWA LAMI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 20 November 2021

BARABARA YA SAME - MKOMAZI KUJENGWA KWA LAMI

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando (wa pili kulia), akionesha na kufafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando (wa pili kulia), akionesha na kufafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando (wa pili kulia), na wataalam wake alipokagua maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Muonekano wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando (kulia), akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46), ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni, wengine (kushoto), ni wataalam wa barabara kutoka mkoa huo.

Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela akitoa shukrani zake kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya (kushoto) na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando (kulia), mara baada ya kukagua ujenzi wa madarara ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu yenye urefu wa (KM 90.19).

Muonekano wa madaraja ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika, madaraja hayo ni miongoni mwa madaraja zaidi ya sita yanayojengwa katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu yenye urefu wa KM 90.19.

Muonekano wa madaraja ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika, madaraja hayo ni miongoni mwa madaraja zaidi ya sita yanayojengwa katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu yenye urefu wa KM 90.19.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Same - Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa (KM 96.46).

Akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo Eng. Kasekenya amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha KM 11.9 ambapo ujenzi utaanzia sehemu ya Mroyo - Ndungu hadi Kihurio. 

Barabara hiyo ambayo inapita pembezoni mwa hifadhi ya taifa ya Mkomazi itachochea na  kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi, kilimo, utalii na biashara kwa wakazi wa tarafa za Gonja, Ndungu, Kihurio, Bendera na Mkomazi wilayani Same na hivyo kukuza uchumi wa wakazi hao. 

 “Tumejipanga kuijenga barabara hii kwa lami na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa”, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Aidha amekagua ujenzi wa madaraja ya Mamba na Yongoma ambayo ujenzi wake umekamilika katika barabara ya Mwembe-Myamba-Ndungu na kuzungumzia umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu hiyo ili itumike wakati wote wa mwaka.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Kilimanjaro Eng. Motta Kyando amesema ujenzi wa madaraja na makalvati katika barabara ya Mwembe hadi Ndungu ni zoezi endelevu hivyo kuwataka wananchi kuepuka kulima karibu na hifadhi ya barabara ili kuepuka mmomonyoko wa udongo.

Naye Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malechela amesema ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi (KM 96.46), na Mwembe-Myamba-Ndungu (KM 90.19), ukikamilika utafungua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Same ambao kwa kiasi kikubwa unategemea shughuli za kilimo cha mazao ya tangawizi na ndizi na kuhuisha  utalii katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


No comments:

Post a Comment