MHE. RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MLEZI WA SKAUTI TANZANIA MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 2 October 2021

MHE. RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MLEZI WA SKAUTI TANZANIA MKOANI DODOMA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha Tuzo Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Salum Hamduni kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono Skauti Tanzania, katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Simiyu Penina Mashimo kulia na Anastandhia Limbe kushoto, wakimvisha Skafu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Oktoba 02, 2021 kwa ajili ya kuhudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania.

No comments:

Post a Comment