DK TEMU ATAKA WATOTO KURITHISHWA UTAMADUNI KWA MAENDELEO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 10 October 2021

DK TEMU ATAKA WATOTO KURITHISHWA UTAMADUNI KWA MAENDELEO

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (katikati), akitazama watalii 270 wanavyoshuka katika ndege ya Edelweiss Airbus A 340 toka Uswis  mara baada ya ndege hiyo kuanza safari zake hapa nchini  (kushoto) ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Uswis hapa nchini Didier  Chassot na kulia ni Mkurugenzi mkuu wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Anga (TCAA) Bw, Hamza Johari.


Abiria wa ndege ya Edelweiss Airbus A 340 wakishuka katika ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), toka Zurich Uswisi. 


Kaimu Mkurugenzi wa KADCO, Christine Mwakatobe (kulia), akimuongoza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa, Makame Mbarawa kwenda kuzindua safari za ndege ya Edelweiss iliyoanza kutoa huduma ya Usafiri kati ya Zurich Uswis na Kilimanjaro na Zanzibar Tanzania.


Na Sixmund J. Begashe

WAZAZI nchini wametakiwa kuwarithisha watoto wao urithi wa kiutamaduni wa asili ya makabila yao ili kujenga kizazi kinacho tambua asili yake na hasa misingi ya Utanzania iliyojengwa kwa mila na desturi za Makabila ya hapa nchini badala ya kuwaachia wakatekwa na tamaduni za kigeni.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utamaduni nchini Dkt Emmanuel Temu, aliemwakilisha Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa (MB) kwenye siku ya utamaduni iliyo andaliwa na Shule ya  Awali  na Msingi ya Mt  JOSEFU iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam na hapa Dkt Temu anasema.

Dkt Temu zaidi ya kuto pongezi kwa shule ya Awali na Msingi ya Mt Josefu, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na  wadau mbalimbali wa Utamaduni ili kuhakikisha dhima ya nchi ya kuwa na kizazi kinacho thamini utamaduni wake inaendelea na kufikiwa kwa kiwango kikubwa zaidi, hivyo amezitaka shule hapa nchini kuhakikisha zinakuwa na program elimishi juu ya utamaduni wa Mtanzania.

Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mt Josefu  Bi Christa Pendo Rweyemamu  amesema kuna licha ya shule yao kufundisha kwa lugha ya kingereza lakini wameona umuhimu wa kuwa na siku ya utamaduni katika shule hiyo kwa kushirikisha wazazi, jamii inayowazuguka na taifa kwa ujumla kwa sababu wazazi walio wengi siku hizi hawapati muda wa kuendeleza asili na tamaduni za kwao hivyo kupelekea watoto wengi kutofahamu, kusahau au kutojua kabisa asili yao ambayo inabeba misingi ya utu, uzalendo na utanzania wetu.

 “Ni wazi hali hiyo ikiachwa inaweza kuhatarisha utambulisho wetu kama watanzania. Hivi leo kutokana na utandawazi, watoto wetu wanajua zaidi kuhusu tamaduni za mataifa mengine kuliko za kwao. Leo hii televisheni, redio na mitandao imejaa filamu na miziki ya Ulaya na Marekan. Wenzetu walitushinda kwa kuwa tamaduni zao zimenakiliwa kwa kina na kuchapishwa maradufu”. Aliongeza Bi Rweyemamu.

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi Alhelmina Joseph licha ya kuupongeza ongozi wa shule hiyo kwa kushirikiana kwa karibu na Makumbusho ya Taifa nchini katika kuwaelimisha watoto na walimu mambo muhimu yanayohusu Utamaduni, ametoa wito kwa Shule na taasisi zingine kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha uhifadhi wa urithi wa kiutamaduni nchini unakuwa endelevu.

“Kwa kweli shule hii ya Awali na  Msingi Mt Josefu hapa Mbezi Beach inastahili pongezi za dhati kabisa, wamekuwa wakishirikiana nasi kwa muda mrefu sasa, kwetu ni wadau muhimu sana katika uhifadhi wa urithi wa Utamaduni, tumejionea hapa watoto wakijifunza mapishi, kuvaa kiasili, nyumba za asili, ngoma za asili na mambomengi, hakika hii haitasahaulika kwa wote tuliofika hapa.” Alisema Bi Joseph.

Mwanafunzi wa shule hiyo, victor Chales na Zuhura Fadhili wamesema licha ya burudani waliyoipata kupitia maonesho hayo pia wameweza kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu makabila yao pamoja na ya watoto wengine jambo linalo wapa ufahamu zaidi juu ya utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni uliopo nchini.

Akielezea umuhimu wa mafunzo hayo ya utamaduni, Mwana wa Mfalme wa Pili wa Kabila la Wahaya Mlangira Katega wapili ameishari serikali kuhakikisha kuanzisha mitaala ya somo la Utamaduni mashuleni ili shule zote nchini zinawafundisha watoto Utamaduni wa Mtanzania ambao upo mbioni kutoweka

“Utamaduni wa kijadi yaani wa kirohoo, ni muhimu sana, hata Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni HANGAI wetu alisema watalii wanakuja wanakaa sikumoja mbili kwa sababu hakuna mambo mengi ya kuona, lakini wakizunguka tunakabila zaidi ya 120, vyakula, ngoma mbalimbali kama tunavyoona leo hapa, mtalii anaweza kukaa mwezi, hivyo nazi kuupongeza uongozi wa shule hii kwa jambo hili kubwa”. Malangira Katego wa Pili

Katika tamasha hili makabila yalishindanishwa kikanda za Kaskazini, Kati, Kusini, Pwani na ya Ziwa katika vipengele mbalimbali kama vile Utawala, Mapishi, mavazi na Kucheza ngoma ambapo ambapo kianda ya Kaskazini ikiibuka msindi wa Jumla baada ya kushinda kipengele cha Mapishi na Mavazi huku Pwani wakishika nafasi ya Pili baada ya kushinda katika Ngoma.

No comments:

Post a Comment