WASANII WA KIZAZI KIPYA KUPAMBA MISS AND MR DEAF AFRICA 2021 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 30 September 2021

WASANII WA KIZAZI KIPYA KUPAMBA MISS AND MR DEAF AFRICA 2021

Msanii, Sholo Mwamba


Na John Mapepele, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Mkichezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wasanii wa kizazi kipya wanatarajia kupamba mashindano ya Urembo na Mitindo kwa Watu Wenye Usikivu Hafifu (Viziwi) Barani Afrika yatakayofanyika Oktoba Mosi, 2021 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es Salaam ili kuongeza hamasa ya shindano hili la kihistoria. 


 Akizungumza kwenye mkutano na Vyombo vya Habari leo Septemba, 30 jijini Dar es Salaam. Dkt, Abbasi amesema kutokana na umuhimu na upekee wa shindano hili Wizara imewachukua   baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakipiga nyimbo za kiasili ili kutambulisha utamadunu wa taifa hili nje ya Tanzania na hatimaye kufungua soko la utalii duniani. 


Amewataja baadhi ya wasanii ambao watatumbuiza katika shindano kuwa ni pamoja na Sholomwamba na Wannestar pia Saraphina na Z anto wa Binti Kiziwi. 


“Ndugu zangu tunashukuru kupata fursa hii adhimu ya kuratibu mashindano ya Afika ya Urembo na Mitindo kwa Watu wenye usikivu hafifu, kama taifa tunakwenda kuyatumia shindano hili kimkakati kutangaza utalii wetu na  vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kuwavutia wageni kutoka kwenye mataifa mbalimbali duniani” amefafanua Dkt. Abbasi


Amesema baada ya kufanya shindano hili Wizara imeratibu washiriki wote kutembelea vivutio na kufanya utalii wa kiutamaduni katika maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo. 


Mashindano haya yanaandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Kituo cha Sanaa Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) yakihusisha vijana wa kike na wa kiume ambao tayari wamewasili jijini Dar es Salaam kujiunga na kambi ya maandalizi kuelekea mashindano hayo kuanzia Septemba 24 hadi 30, 2021.


Jumla ya washiriki takribani 60 kutoka nchi 11 Barani Afrika wameshawasili nchini tayari kwa mpambano huo wa kukata na shoka, nchi hizo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Siera Leon, Uganda, Kenya, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Senegal, Sudani Kusini na Zimbabwe. 


No comments:

Post a Comment