Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kiuchumi wanufaika wa mpango huo waliorasimishiwa ardhi yao kwa kupatiwa hati miliki za kimila katika Kijiji cha Lugodalutali Kata ya Igombavanu, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa Juni Mosi, 2021.
Walioshiriki mafunzo hayo walikuwa 395 ambapo walifundishwa jinsi ya kutumia hati miliki kuweka kama dhamana kukopea fedha benki na taasisi zingine za fedha ii kuinua mitaji ya miradi yao, kanuni bora za kilimo ili kupata mavuno mengi kwa heka moja, kuthaminisha rasilimali zao na hasa ardhi, jinsi ya kuweka kumbukumbu za mahesabu ya miradi yao, umuhimu wa kujiunga na ushirika na faida zake na faida za kuweka akiba benki na mikopo inayotolewa na benki hizo.
Maofisa walioshiriki kutoa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu ni;Maofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ambao ni Afisa Ardhi Mteule, Leonard Jaka, Afisa Ushirika, Pili Mwaipaja, Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka, Afisa Ufugaji Nyuki, Hamisi Hassan, Afisa Maendeleo ya Jamii, Joha Kambala na Afisa Upimaji Ardhi Imamu Sherukindo.
Kwa upande wa benki waliotoa mafunzo ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Gasper Mlala, Afisa Mikopo wa Benki ya Posta, TPB, Japhet Peter na Prosper Peter wa Benki ya Mucoba ambao kila mmoja alieleza masharti ya kujiunga, masharti ya ukopaji na faida zake. Benki zote hizo zinaruhusu kuweka hati miliki za kimila kuweka kama dhamana kukopa fedha.
Awali mafunzo hayo ambayo wengi waliyafurahia na kuomba Mkurabita kuwapelekea tena siku nyingine, yalifunguliwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Sailas Kiwuyo na kupata baraka za mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Igombavanu, Veronica Kilongumtwa.
Wananchi wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mufindi, Joha Kambala akitia dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa Kobo.
Msaidizi Upimaji Ardhi wa Kijiji cha Lugodalutali, Felister Choga akiingiza taarifa za dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa wa Kobo.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mkurabita, Anthony Temu akiingiza taarifa za dodoso kwenye simu janja kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji taarifa wa Kobo.
Kwaya ya Mashahidi wa Uganda ikitumbuiza wakati mafunzo hayo.
Prosper Peter wa Benki ya Mucoba akiwaeleza wananchi umuhimu wa kuwa na tabia ya kuweka akiba fedha zao benki, kutumia hati miliki za kimila kukopa kupanua wigo wa miradi yao.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Gasper Mlala akiwahamasisha wananchi kujiunga na benki hiyo kwa kutoa kiingilio cha sh. 5000 na kuahidi kufungua wakala wa benki hiyo katika kijiji hicho.
Afisa Mikopo wa Benki ya Posta, TPB, Japhet Peter akielezea masharti ya kujiunga na benki hiyo, mikopo wanayotoa na faida zake.
Afisa Kilimo, Mwamini Mwakyaka akiwafundisha kanuni za kilimo na hasa kilimo bora cha zao la alizeti.
Afisa Upimaji Ardhi Imamu Sherukindo. akielezea faida za kurasimisha ardhi kwa kuiongezea thamani pamoja na kupata hati miliki.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Joha Kambala akiwafundisha jinsi ya kuunda vikundi na faida zake ikiwemo urahisi wa kupata mikopo na misaada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment