Na Mwandishi Wetu, Singida
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utaratibu wa kuunganishiwa umeme kwa Bei ya Sh.27,000/= tu.
Akizungumza jana katika zoezi hilo la utoaji wa elimu hiyo wilayani Manyoni, Afisa Masoko wa Shirika hilo kutoka Makao Makuu, Jennifer Mgendi alisema uhamasishaji huo unafanyika mkoa mzima wa Singida na wilaya zake zote.
"Uhamasishaji huu tunaufanya mkoa mzima na wilaya zake zote lengo ni kuwaelimisha wananchi ambao ndio wateja wetu wauelewe na wawatumia wakandarasi waliosajiliwa ili waweze kuwafungia umeme kwenye nyumba zao," alisema Mgendi.
Aidha Mgendi alisema kuwa kwa wale wenye nyumba zenye ukubwa mdogo watumie kifaa cha Umeta au Umeme Tayari ili wapunguze gharama za kusuka nyaya kwenye nyumba zao.
Zoezi hilo la Uhamasishaji Mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) III, mzunguko wa Kwanza na Mradi Jazilizi unaoendelea mkoani hapa unafanywa na Afisa Masoko huyo kutoja Tanesco makao makuu, Jennifer Mgendi kwa kushirikiana na Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Witness Msumba.
No comments:
Post a Comment