KAMATI KUU YA CCM YAKUKUTANA DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 21 June 2021

KAMATI KUU YA CCM YAKUKUTANA DODOMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akizungumza wakati wa Kufungua kikao Cha Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa makao makuu ya CCM White House jijini Dodoma (kulia) Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt Abdallah Sadala Mabodi,(Kushoto) Ndg Christina Mdeme Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara. 

Sehemu ya Wajumbe wa sekretariet wakifuatilia kikao hicho. 

katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndg Daniel Chongolo akizungumza wakati wa Kufungua kikao Cha Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa makao makuu ya CCM White House jijini Dodoma Leo.

KAMATI Kuu ya Halmashauri  Kuu ya CCM inatarajiwa kukutana Jumanne Juni 22, 2021 chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho  kimetanguliwa na kikao cha Secretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Daniel Chongolo kimefanyika katika ukumbi wa NEC White House Jijini Dodoma. 

"Ni kweli Jumanne 22 Juni 2021 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza kikao cha kawaida cha kamati Kuu, maandalizi yote yamekamilika, ni kikao cha kawaida cha Kikatiba" *Shaka Hamdu Shaka Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

No comments:

Post a Comment