Meneja Vifaa Vya Intaneti wa Tigo Mkumbo Myonga Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) mara baada ya uzinduzi wa uzindua simu janja aina ya Infinix Hot 10 play ambazo zitakua zikipatikana nchi nzima.Kulia kwake ni Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa.
Mkumbo Myonga, Meneja Vifaa Vya Intaneti wa Tigo alisema: “Mkakati wa makubaliano baina ya Tigo na Infinix, yanalenga kuendeleza bidhaa hiyo ambapo kwa sasa katika soko la Tanzania kuna mahitaji makubwa ya huduma ya teknolojia ya 4G kwenye simu.
"Tumetambulisha Infinix Hot 10 play kwa ajili ya kuwaaminisha wateja wetu wote nchini kutumia mtandao wa 4G".
Myonga pia aliongeza katika uzinduzi huo wa Infinix Hot 10 play, utasaidia kuongeza thamani sokoni kwa wafanyabiashara kutokana na ubora wa bidhaa hiyo kwa Watanzania wote.
“Mbali na kuwaletea wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na bei rahisi, Infinix Hot 10 play ni sehemu ya mikakati ya kuendelea kuleta bidhaa nzuri zaidi nchini kwa ajili ya magaeuzi ya kidijitali nchini,".
Kwa mujibu wa Myonga “Simu hizo kwa sasa zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na simu itakuwa ofa ya bando ya GB 78, kwa mwaka mzima.“
Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema: “Infinix Hot Play ina kadi maalumu ya Helio G35 Chip ambayo ina michezo mbalimbali kwa ajili ya mtumiaji.
"Uwezo wake wa betri ni 6000 mAh ambayo inakaa saa 24 na utacheza game muda wote, Infinix hot 10 play ina uwezo wa 6.82 kutazama sinema na kupiga picha kamera ina uwezo wake ni 13MP, inatumia taa ya flashi, Hot 10 play inapatikana katika maduka yote ya Infinix na maduka ya Tigo nchi nzima”
No comments:
Post a Comment