Vedasto Msungu. |
SALAMU ZA POLE
Dodoma – Februari 18, 2021
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwandishi wa Habari wa vituo vya ITV/Radio One Stereo Vedasto Msungu, ambaye amefariki dunia Februari 17, 2021 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipokua akipatiwa matibabu.
“Hili ni pigo kwa wadau wa tasnia ya Habari nchini, tutamkumbuka Vedasto Msungu kwa kazi yake ya kuelimisha umma kupitia vipindi vyake vya utalii pamoja na uhifadhi wa mazingira,” alisema Mhe. Bashungwa.
Marehemu Vedasto Msungu atakumbukwa kwa kazi zake za uandishi wa habari hasa kwa kuitangaza sekta ya utalii ambayo ilimesaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Mhe. Bashungwa ametoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki, Waandishi wa Habari, uongozi na wafanyakazi vituo vya ITV/Radio One Stereo, Chama cha Waandishi wa Habari Morogoro pamoja na wadau wote wa tasnia ya habari. Pia anawaombea wote kwa Mwenyezi Mungu, wapate nguvu na moyo wa ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Imetolewa na
Shamimu Nyaki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
No comments:
Post a Comment