Mratibu wa Tiba asili
Mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya siku moja
ya wadau wa tiba asili na bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa niaba
ya Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro
Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
1. Muwakilishi
wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma, Prof. Samweli Kabote akitoa
shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya hutuba yake ya ufunguzi,
Mgeni rasmi na ujumbe
aliofuatana nao wakitembelea mabanda ya maonesho ya waganga wa tiba asili kuona
bidhaa mbalimbali waliozokuja kuonesha kwenye maonesho hayo toka mikoa
mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mhe, Fredirick Sumaye akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa waoneshaji kutoka shirika la SAT bwana Allen alipotembelea maonesho hayo kuona bidhaa mbalimbali za wataalamu wa Tiba Asili.
Na Calvin Gwabara, Morogoro
SERIKALI Mkoa wa Morogoro, na hasa vitengo vya Uchumi na Mali Asili vimewahakikishia wadau wa tiba asili kuwa wakotayari kushirikiana nao kikamilifu ili kuona kuwa mimea dawa nchini inatumika kwa uangalifu na kwa mpango endelevu.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa niaba yake na Mratibu wa Tiba asili mkoa wa Morogoro Dkt. Ngalula Wille wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya siku moja ya wadau wa tiba asilina bidhaa zake yaliyofanyika mkoani Morogoro na kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Mradi wa GRILI.
Mratibu huyo wa tiba asili mkoa wa Morogoro amewataka wazalishaji wa bidhaa hzo za mimea dawa kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa mlipuko kama COVID-19, waone namna gani watatengeneza dawa ilikusaidia jamii kukabiliana na majanga kama haya yanayiweza kujitokeza.
"Nimefurahishwa sana na taarifa kwamba maonesho haya yamendaliwa na Chuo chetucha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kurugenzi yake ya Uzamili kitengo chake cha Uhaulishaji wa tekinolojia pamoja na mradi wa utafiti wa GRILI Hii inatokana na uzoefu na ueledi walionao kwenye masuala ya utafiti na Biashara za aina hii zikiwemo za bidhaa zinazotokana na mimea dawa hivyo ni matumaini yangu kuwa maonesho haya yataangalia pia namna yakupunguza changamoto za uzalishaji na za kibiashara zilizopo na zinazoweza kujitokeza katika biashara nzima ya bidhaa za mimea dawa" alisema Dkt. Ngalula.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda alisema kuwa ingawa kwenye kanuni za biashara ya madawa kuna mitizamo tofauti kuhusu kutangaza dawa za mimea zitokanazona mimea tiba, lakini ukweli ni kwamba bilikujitangaza, wateja hawatatambua biashara za bidhaa na soko.
“Biashara hii iko pia kwenye biashara ya huduma zinakuzwa sana na watoa huduma wenyewe hivyo hii sio tu yatatangaza biashara zao bali pia yatatangaza watoa huuma wenyewe na kauli zao kwa wateja ni muhimu sana ili waweze kupata masoko ya bidhaa na huduma zao hvyo lengo la maonesho haya nikuwakutanisha wazalishaji, wasambazaji, watengenezaji na wanunuzi wa bidhaa za mimea dawa” alifafanua Prof Mhairwa.
Aliongeza "Napenda niwahakikishie wadau hawawanaozalisha dawa zinazotokana na mimeadawa kwamba, Chuo Chetu chaSUA, kupitia kurugenzi ya Uzamili, Utafiti,Uhaulishaji waTekinolojia na Ushauri wa Kitaalaamu, kwakushirikiana na Watafiti tulionao na wamasuala ya kisayansi na tekinolojia, na wale wa masuala ya biashara, tutaendelakushirikiana bega kwa bega na wajasiriamalihawa ili kuboresha bidhaa wanazozalishatukishirikiana na wadau wengine katika sektahii kwa kadri uwezo wetu utakavyoturuhusu".
Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Ras wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia Prof. Samweli Kabote kwa niaba ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema wamepokea ushauri na maelekezo yote aliyoyatoa mgeni rasmi na kuahidi kutafanyia kazi na kushirikiana nao zaidi katika kuboresha bidhaa za tiba asili kufikia viwango vya kimataifa ili kuinua uchumi wao na taifa sambamba na kuboresha afya za jamii.
Alisema maonesho hayo ni mwanzo wa maonesho ya fursa nyingi za katika tafiti za mimea dawa na tiba asili na kuwataka wataalamu wa tiba asili kuwatumia watafiti wa SUA kwenye mambo mbalimbali yanayohitaji sayansi zaidi.
Kwa pande wake Mkuu wa Mradi wa GRILI ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo Dkt. Faith Mabiki amesema tafiti nyingi zimefanywa na watafiti wa SUA kwenye Mradi huo kwenye masuala ya miti dawa na kupata matokeo mazuri ambayo yatassidia kwenye kuongeza thamani na kuboresha tiba asili na uendelevu wake.
Dkt. Mabiki ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wote wa Tiba asili nchini kushiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Ubunifu katika tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye Ndaki ya Solomon Mahlangu ya Sayansi na Elimu kwenye kampasi ya Mazimbu kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 7:00 Mchana.
Amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utakuwa mwanzo mzuri wa kupata
jukwaa la pamoja kati ya wadau wote wa tuba asili na wasimamaizi wa tiba asili
upande wa serikali kujadiliana kwa pamoja mambo muhimu ya kuendeleza sekta hiyo
ambayo imeshika kasi sana ikilinganishwa na huko nyuma kabla ya Ugonjwa wa
Covid-19.
No comments:
Post a Comment