Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na watendaji na wananchi ambapo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida DC Rashid Mwandoa kumvua cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi Charles Mtiko kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu .
Na Mwandishi Wetu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida Dc Ndugu Rashid Mwandoa kumvua cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi Charles Mtiko Kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu (Two in one).
Vifaa vinavyodaiwa kuibiwa ni mbao za kupauliwa, Saruji na nondo ambayo thamani yake bado haijafahamika.
Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi ambapo watuhumiwa wote wako Polisi.
Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanao tuhumiwa kwa ubadhilifu na atakaye bainika atashughulikiwa vilivyo.
Nchimbi amewataka viongozi wa Serikali kusimamia miradi na kuwa waminifu katika fedha zinazoletwa na Serikali ya Rais Magufuli pia wananchi wa hakikishe wanalinda mali hizo kwani miradi hiyo ni kwa ajili ya maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment