OFISI YA ARDHI RUKWA YAWATAHADHARISHA WALIOVAMIA MAENEO YA UMMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 5 November 2020

OFISI YA ARDHI RUKWA YAWATAHADHARISHA WALIOVAMIA MAENEO YA UMMA

Mmoja wa Wananchi akitoa maelezo ya mgogoro wake katika kiwanja kilichovamiwa baada ya kukutana na Timu ya Uhakiki wa maeneo ya wazi ililopita katika mtaa anaoishi mzee na huo hali iliyompelekea Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga kumsikiliza na kuchukua malalamiko hayo kwa nia ya kuyafanyia kazi. 

Na Abdulrahman Salim, Rukwa

OFISI ya Ardhi Mkoa wa Rukwa inaendelea na zoezi la kufanya uhakiki wa maeneo ya wazi na maeneo ya umma yaliyoorodheshwa kwa mujibu wa ramani za mipango miji za halmashauri za mkoa huo ili kubaini endapo kuna uvamizi umefanyika katika maeneo hayo.


Akiongea kuhusiana na zoezi hilo Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kupata orodha kamili ya meneo ya wazi ili yaweze kutambulika rasmi huku akiwaonya wananchi waliovamia katika maeneo hayo.


“Kwa maeneo ambayo yatakuwa yamevamiwa, kutakuwa hakuna namna ya kufanya isipokuwa wavamizi wataondolewa ili kupisha maeneo ya wazi kwasababu yanatakiwa yalindwe kwa nguvu zote, na maeneo ambayo yapo salama mpaka sasa hivi tutahakikisha mipaka yake inawekwa bayan ana wananchi watatakiwa waiheshimu,” Alisema.


Aidha aliongeza kuwa baada ya kupata orodha ya kamili ya maeneo hayo atakabidhiwa Mkurugenzi ili aweze kuyaandalia hati kwaajili ya ulinzi wa maeneo hayo kwa siku za usoni.

No comments:

Post a Comment