RC MNDEME ACHANGIA KANISA TANI TANO ZA SARUJI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 11 October 2020

RC MNDEME ACHANGIA KANISA TANI TANO ZA SARUJI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Christina Mndeme.


MKUU
wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme  amewaomba viongozi wa Dini kuombea nchi  ya Tanzania amani kuelekea uchaguzi  mkuu unaotarajia kufanyika  Oktoba 28,2020.

Mndeme ameyasema hayo wakati anazungumza katika maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Menonite  mjini Songea mkoani Ruvuma.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amechangia ujenzi wa kanisa hilo tani tano za saruji zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu.

“Endeleeni kuiombea nchi yetu tunasali hapa kwa sababu kuna amani  wengine wanakimbia na masanduku na watoto  kwasababu hakuna amani katika nchi zao”,alisisitiza Mndeme.

Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla kuendelea  kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli pamoja na wasaidizi wake ili nchi ya Tanzania ipate maendeleo zaidi katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Moroviani Usharika wa Songea mjini Selemani Nzyemba akizungumza kwa niaba ya Mchungaji wa Kanisa la Menonite amemshukuru Mkuu wa Mkoa na timu yake kwa kwa msaada wa vifaa vya ujenzi.

Amesema msaada huo ni mkubwa kwa kanisa hilo ambao utasaidia kuendeleza ujenzi na kwamba pia amemshukuru kwa kuacha majukumu yake na kufika kushiriki katika  ibada ya kuazimisha mwaka mmoja tangu kuanzisha kanisa hilo mjini Songea. 

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma


No comments:

Post a Comment