![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Kahama - Anamringi Macha (mwenye Miwani) akipokea msaada wa vitanda, magodoro na mashuka kutoka kwa Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB - Emmanuel Akonaay kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Ushetu - Kahama.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa wakati Benki hiyo ikizindua huduma mpya tatu za kibabe katika maeneo mbali mbali nchini; Namba ya WhatsApp 0747333444, njia ya digitali ya kutoa maoni kwa mfumo wa kuscan QR pamoja na mfumo wa kurudisha token za umeme (token retrieval) wakati wakiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Hospitali mpya ya Halmashauri ya wilaya ya Tarime iliyopo Nyamwanga ilikabidhiwa vitanda saba vikiwemo viwili vya kujifungulia na magodoro. Akipokea msaada huo Katibu Tawala wa wilaya ya Tarime, John Marwa alisema msaada huo utaboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya watu 300,000 wakiwemo wamama wajawazito.
Katika hatua nyingine, Benki hiyo pia imetoa msaada wa meza na viti 50 kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Mkalapa iliyopo Ndanda wilaya ya Masasi, ili kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo.
Benki ya NMB kupitia kitengo chake cha Uwajibikaji kwa Jamii, imekua na utaratibu wa kurejesha sehemu ya faida yake ya asilimia moja kwa jamii kusaidia katika sekta ya afya, elimu na majanga.
No comments:
Post a Comment