![]() |
Mradi
wa ujenzi wa nyumba saba za wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Mbinga Mji
ambao umegharimu shilingi milioni 350.
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Grace Quintine ambaye amesimamia miradi hiyo kwa uaminifu mkubwa.
Mradi wa ujenzi wa
jengo la Halmashauri ya Mji Mbinga ambao serikali ya awamu ya Tano imetoa zaidi
ya shilingi bilioni 2.9 kutekeleza mradi
huu.
HALMASHAURI ya Mji wa
Mbinga Mkoani Ruvuma, imetumia zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizotolewa na
serikali kwa ajili ya kutekeleza mradi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Mji
na nyumba saba za wakuu wa Idara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo Grace Quintine amesema Halmashauri yake katika
kipindi cha mwaka 2019/2020 ilipokea kiasi cha sh. milioni 350 kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba saba za wakuu wa Idara ambazo ujenzi wake umekamilika.
“Mradi huu wa nyumba za watumishi
utasaidia sana wakuu wa Idara, badala ya Halmashauri kuwalipia pango la nyumba,
tutakuwa tumewasaidia nyumba hizi, mradi umefanyika kwa 'force account' na Msimamizi
Mkuu wa mradi alikuwa ni TARURA’, alisema Quintine.
Amesema serikali ya Awamu ya Tano pia
imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.9 ambazo zimetumika kutekeleza mradi wa jengo
la Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambalo limeanza kutumika hivyo kuboresha
mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina
Mndeme kwa niaba ya wananchi wa Mbinga, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa
kuruhusu kiasi hicho cha mabilioni ya fedha yaliyowezesha kujengwa jengo bora
la Halmashauri ya Mji wa Mbinga na nyumba saba za watumishi.
“Tuna kila sababu ya kumshukuru Rais
wetu kwa zawadi hii kubwa, kwa niaba ya serikali nawapongeza wana Mbinga Mji
kwa kupata jengo hili zuri na rafiki la kutolea huduma,’’ alisisitiza Mndeme.
Imeandikwa
na Albano Midelo
Afisa
Habari wa Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment