WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI BAADA YA KUSAMBAZIWA MAJI VIJIJINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 17 September 2020

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI BAADA YA KUSAMBAZIWA MAJI VIJIJINI

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akiongea na baadhi ya wataalamu baada ya kuona ujenzi wa tenki la maji katika mradi wa P4R katika kata ya Mtowisa.


Mwonekano wa maji yanayotiririka kutoka katika milima ya Lyamba Lyamfipa na kumwaga maji yake katika mto Nteteze ambapo serikali imeboresha chanzo hicho ili kuwawezesha wananchi kupata maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani na kwaajili ya kilimo katika skimu ya umwagiliaji kwa kipindi chote cha mwaka. 

WANANCHI wa vijiji vya Ng’ongo na Mtowisa katika Kata ya Mtowisa, Wilayani Sumbawanga, Mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya mradi wa maji wa lipa kulingana na matokeo (P4R) katika vijiji vinne vya Kata ya Mtowisa utakaohudumia wakazi zaid ya 11,000.

Wanachi hao wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji hali ambayo imekuwa ikiwazuia kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo na hivyo ukamilifu wa mradi huo ambao umegharimu Zaidi ya shilingi milioni 464 utakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hiyo.


Abedi Saidi ni Mkazi wa Kijiji cha mtowisa aliyekuwa akitembea kwa masaa kadhaa kutafuta maji alisema, “Ni mbali kutoka Mtowisa hadi hapa Ng’ongo kuna kaumbali kidogo kwa miguu ni masaa mawili, mradi huu ukikamilika wananchi watafurahi sana, kwasababu mradi waliokuwa anatumia ni wa zamani halafu umechakaa yani watu wanahangaika sana, yaani huu mradi tumeufurahia na tutautunza sana.”


Aidha, Mwanakijiji Christian Kapele aliorodhesha faida zitakazopatikana baada ya mradi huo kuisha ikiwemo kupata maji ya uhakika katika hospitali mpya ya Wilaya Sumbawanga iliyopo katika kata ya Mtowisa Pamoja na kufikisha maji katika vijiji vinne ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikihangaika kutafuta maji.


“Tunamwombea Muheshimiwa Magufuli, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanakijiji wa Ng’ongo tunaahidi kwamba tutafanya chini na juu apite nafasi kwa kura zote ili aweze kutuendeleza kwenye hii miradi yet una tunashukuru sana huyu mzee wetu ametusaidia maji katika kata yetu, na umeme na hivyo tunamuombea aweze kushinda katika uchaguzi huu,” Alisema.


Wakati alipomaliza kutemebelea mradi huo wa P4R Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwani ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya wananchi kwakuwa maji hayo hayatumiki tu majumbani lakini pia yanatumika katika mradi wa skimu ya umwagiliaji katika kata hiyo ya Mtowisa.


“Niwaombe wanakijiji wa vijiji hivi vinne watunze mradi huu, watunze mazingira, msifugie na kulisha katika vyanzo hivi, lakini pia huko juu kwenye vijiji vilivyopo kweny ukanda wa Sumbawanga watunze vyanzo vya maji wasichome misitu hovyo, wasifyeke misitu wala wasifuge katika maeneo ya vyanzo vya maji, vinginevyo watu wanaoishi katika bonde hili la ziwa Rukwa watapata athari kubwa ya kutopata maji safi na salama lakini pia ziwa Rukwa litakuwa katika hatari ya kutoweka, tutunze vyanzo ili maji yatutunze,” Alimalizia.

No comments:

Post a Comment