TANZIA: MWANAMUZIKI MZEE SAIDI MABERA AFARIKI DUNIA DAR - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 29 September 2020

TANZIA: MWANAMUZIKI MZEE SAIDI MABERA AFARIKI DUNIA DAR

Marehemu Mzee Saidi Mabera wa Msondo Ngoma Music Band.

MWANAMUZIKI MZEE SAIDI MABERA WA MSONDO NGOMA MUSIC BAND AMEFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM. Mwanamziki huyo mahili na mpiga gitaa Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia Septemba 29, 2020. Mzee Mabera alikuwa mwanamuziki wa bendi kongwe barani afrika 'Msondo Ngoma Music band' yenye makao yake nchi Tanzania.

Marehemu alijiunga na bendi hiyo mwaka 1973 na ajawahi kuhama, ndiye mwanamziki pekee mkongwe nchini Tanzania aliyeweka rekodi ya kutulia katika bendi moja bila kuhama. Marehemu Saidi Mabera atakumbukwa daima katika mchango wake kimuziki na ustadi wake wa upigaji wa gitaa la solo.
Mungu amlaze mahala pema pema peponi

No comments:

Post a Comment