Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wajumbe wa Menejiment ya Wizara hiyo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati anawaaga kuanza ziara ya kutembelea mradi ujenzi wa Reli ya ya Kisasa (SGR) ili kujionea maendeleo yake ikizingatiwa Wizara hiyo ndiyo yenye dhamana kuisemea Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika wakitembelea handaki la nne eneo la Kilosa mkoani Morogoro kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaojengwa kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza.

Na Eleuteri Mangi,
Morogoro
UJENZI wa Reli ya ya
Kisasa (SGR) nchini unalenga kuleta maendeleo ya watu kwa kurahisisha muda wa
usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo ambapo kutoka Dar es Salaam hadi
Morogoro itakuwa ni saa tatu au dakika 90 hatua itakayopunguza muda mwingi unaopotea
barabarani na kuwafanya wananchi kuwahi kufanyakazi nyingine za maendeleo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan
Abbasi amesema hayo leo Ihumwa jijini Dodoma wakati anawaaga Menejimenti ya
Wizara hiyo kuanza ziara ya kutembelea mradi wa SGR ili kujionea maendeleo yake
ikizingatiwa hiyo ndiyo ni Wizara yenye dhamana kuisemea Serikali kupitia Idara
ya Habari (MAELEZO).
“Wizara ya Habari ni
Wizara muhimu sana katika nchi yetu na mradi huu pia. Ndiyo wizara yenye
dhamana na habari kwa maana hiyo tumekuwa tukiutangaza sana, na kuukiulinda mradi
huu ili kuwaonesha watanzania nini kinaendelea kwenye huu mradi” alisema Dkt.
Abbasi.
Dkt. Abbasi amesema
kuwa Tanzania ipo makini kuwekeza kwenye mambo ambayo ni muhimu katika kuleta
manufaa na maendeleo ya watu na kusisitiza kuwa ni utamaduni mpya kwenye nchi
yetu kuwa na taifa la wachapakazi, kuwa watanzania wanaojiamini na kuwa watu
wanaopenda mambo mazuri ambayo yanaletwa na Serikali kwa manufaa ya wananchi
wake.
“Tunaposema huu
ujenzi wa reli ni kitu, ndiyo ni kitu, reli ya SGR ni kitu kinachokwenda kuleta
maendeleo ya watu. Utakapoweza kusafiri kwa saa tatu au dakika 90 Dar es Salaam
hadi Morogoro umepunguza muda mwingi wa kupoteza barabarani na kuwahi kwenda
kufanyakazi”alisisitiza Dkt. Abbasi.
Mradi huo ni moja miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini na kuwa miongoni mwa miradi mikubwa Afrika ambapo Serikali imewekeza trakriban trilioni saba (07) kwa kipande cha Dar es Salaam, Morogoro hadi Mkutupora mkoani Singida ambapo kipande cha Morogoro hadi Dodoma kimefikia asilimia 42 hadi kukamilika kwake.
Muonekano wa moja ya mahandaki itakapokuwa inapita Reli ya Kisasa (SGR) eneo la Kilosa Mkoani Morogoro.
Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika wakitembelea handaki la nne eneo la Kilosa mkoani Morogoro kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaojengwa kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Mwanza.
Akitoa maelezo ya
mradi huo kwa mwajumbe wa menejimenti ya wizara hiyo, Meneja wa mradi kipande
cha Morogoro hadi Mkakutupora mkoani Singida Mhandisi Mteshi Tito amesema reli
hiyo itatumiwa na treni ya abiria ambayo itakuwa na mwendo wa kasi ya kilometa
160 kwa saa na ya mizigo itatumia saa moja kwa kilometa 120 hatua inayopelekea mradi
huo kuwekewa uzio kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kuepusha muingiliano wa watu
wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Mhandisi Mteshi ameongeza
kuwa kipande cha reli ya SGR kati ya Morogoro na Mkutupora Singida kina jumla
ya km 422 ambapo km 336 zinajumuisha njia kuu na km 86 sehemu za kupishania
treni.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Menejiment ya Wizara hiyo imeshuhudia na
kujionea wenyewe uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali na kuongeza
itakapokamilika reli hiyo kutakuwa na usafiri wa uhakika kutoka Dar es Salaam
hadi Mkutupora Singida ambayo itakuwa na manufaa kiuchumi katika sekta ya
usafirishaji.
No comments:
Post a Comment