Msanii Zuchu a.k.a 'Chuchu'. |
WASANII wengi mastaa Tanzania wameonekana kumkubali Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli hadi kumsapoti kwa kutunga nyingo kuonesha mambo mazuri na makubwa aliyofanya kipindi cha miaka mitano yake akiwa madarakani.
Wasanii nguli kama Ali Kiba ameimba wimbo 'Number 1' kumsapoti mgombea huyo wa urais kupitia CCM, Diamond Platinum akimfagilia katika wimbo 'Magufuli Baba Laoooo' huku nguli Komando Hamza Kalala akiibuka na wimbo wa 'Huyoo Magufuli Wamemchokoza Wenyewe Sasa Waiona Ng'hondo wafunga Virago'.
Kwa upande wake msanii Harmonize ameimba 'Magufuli na Ile Singeli ya Beat ya Hajanikomoa', Zuchu a.k.a 'Chuchu', msanii Rayvanny na wengine wengi wameiomba nyimbo kumsapoti mgombea huyo wa nafasi ya urais kupitia CCM.
No comments:
Post a Comment