Kada wa Chama cha Mapinduzi Onesti Male akipokea Fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Miriam Kaaya za kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mtia nia ya Ubunge jimbo la Vunjo akisalimiana na Classmet wake nje ya ofisi za CCM wilaya ya Moshi Vijijini mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge katika jimbo la Vunjo.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Vunjo, Onesti Male akionesha fomu zake mara baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi.
Na Dixon Busagaga, Moshi
KADA wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Onesti Male amesema mwaka huu utabili unaenda kutimia baada ya
kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia Chama
cha Mapinduzi.
Male ambaye ni
mfanyabiashara na Mkufunzi amezungumza muda mfupi baada ya kutoka ofisi za
Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Moshi kutimiza takwa la kwanza la katiba ya CCM
la kwenda kuchukua fomu kuijaza na kuirudisha.
No comments:
Post a Comment