MAKADA CCM WAENDELEA KUPIGANA VIKUMBO...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 July 2020

MAKADA CCM WAENDELEA KUPIGANA VIKUMBO...!

Katibu wa CCM Korogwe Mji Fatma Shomary akimkabidhi Grace Stephen Ngonyani.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu leo  amechukua fomu ya kuomba ridhaa tena ya  nafasi ya  Ubunge wa  jimbo la  Geita Mjini,   Naibu Waziri Kanyasu amekabidhiwa  fomu hiyo na Katibu wa CCM wilaya ya Geita, Mwinyikheri Baraza  katika ofisi za CCM wilaya ya Geita  katika mkoa wa Geita.

Waziri wa Mambo ya Ndani Laurance Masha(kulia) akichukua fomu kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi-CCM kupeperusha bendera jimbo la Sengerema.
Mhariri Msaidizi Maudhui ya Mtandao Uhuru Digital, Jane Mihanji akichukua fomu Kugombea Jimbo la Mlimba Morogoro.

Baruan Muhuza (kushoto) akichukua fomu kuwania Jimbo la Kigoma Mjini kupitia CCM.

Mtangazaji na Mwandishi wa Habari nguli nchini Ndugu, Jacob Tesha akichukua fomu Ofisi za CCM Wilaya ya Moshi, kuwania ubunge Jimbo la Moshi mjini. 

Eng. Ezra Chiwelesa (kushoto) mgombea ubunge Jimbo la Biharamuro CCM akimkabidhi Fomu Katibu wa CCM Wilaya ya Biharamulo Bi. Adia Rashid Mamu Kulia baada ya kuichukua fomu hiyo julai 14 mwaka huu dirisha la uchukuaji fomu lilipofunguliwa rasmi na kuirejesha leo julai 15,mwaka huu akiwa ameijaza.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Biharamulo Bi. Adia Rashid Mamu Kulia akimkabidhi fumu ya kugombea ubunge Bw. Idrissa Songoro kushoto akiwa amefika ofisi hapo kuchukua fomu na kuingia kwenye idadi ya watia nia 40 wa wilaya hiyo hadi Julai 15, mwaka huu.




No comments:

Post a Comment