NEC YATOA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2020 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 July 2020

NEC YATOA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2020

Jaji wa Rufaa (Mst.) Semistocles S. Kaijage.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Uchaguzi Mkuu mwa mwaka  2020 wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani utafanyika 28 Oktoba, 2020.

Akitoa ratiba hiyo, leo jijini Dar es Salaam kwa wanahabari, Mwenyekiti wa tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst.) Semistocles S. Kaijage amesema taarifa hiyo ya tume imetolewa kwa Mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 41(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na vifungu vya 35B (1), (37) (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 48 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Akifafanua zaidi amesema, Uteuzi wa Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Ubunge, na
Udiwani utafanyika 25 Agosti, 2020, huku kampeni kwa wagombea wateule zikitarajia kuanza 26 Agosti, 2020 hadi 27 Oktoba, 2020.

"...Tunapenda kuwajulisha Wananchi kuwa Siku ya Uchaguzi itakuwa ni 28 Oktoba, 2020," alisema  Jaji Kaijage.

No comments:

Post a Comment