HUSEIN MWINYI KUPEPERUSHA BENDERA YA URAIS CCM, JPM HUYOOO...TENA
|
Dk. Hussein Mwinyi. |
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala nchini Tanzania, imemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia CCM Zanzibar. Waziri Mwinyi ameibuka mshindi bajada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili.
|
Dk. John Pombe Magufuli. |
Halmashauri Kuu ya CCM pia imempendekeza, Mwenyekiti wa Chama hicho taifa Dk. John Pombe Magufuli kupeperusha bendera ya CCM nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo Dk. Magufuli ataidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 11-12, 2020 jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment