Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (wa tatu kushoto)akikabidhi saruji mifuko 30 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Musimi katika Kata ya Sepuka wilayani Ikungi jana.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kulia) akizungumza na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kinyampembee wakati akikagua ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akishiriki mazishi ya Mzee Maarufu wa Kata ya Sepuka aliyefariki juzi.
Na DottoMwaibale, Singida.
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa msaada wa saruji mifuko 30 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Musimi katika Kata ya Sepuka wilayani Ikungi.
Akizungumza wakati akitoa msaada huo jana, Kingu alisema anatimiza ahadi yake baada ya kuombwa kusaidia ujenzi wa kanisa hilo.
" Mapema mwaka huu uongozi wa kanisa hilo uliniomba niwasaidie mifuko 100 ya saruji kwa aliji ya ujenzi wa kanisa hilo ambapo leo hii nimetoa mifuko 30 ili kuendelea na ufyatuaji wa matofari" alisema Kingu.
Alisema saruji hiyo ataitoa kwa awamu tatu ambapo ameanza na mifuko hiyo 30 ili kazi iweze kuendelea na baadae atamalizia kutoa hiyo mingine.
Kingu alisema amekuwa akisaidia jamii na makundi mengine katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa makanisa na misikiti.
Pamoja na mambo mengine Kingu alikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kinyampembee na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo ili kujua nini kinahitajika ili kusukuma ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment