Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kata ya Nyakibimbili alipokagua barabara ya Kyaka-Kanazi-Kietema Km 60.65 ambayo mchakato wa kuijenga kwa lami umeanza. |
Muonekano wa barabara ya Kyaka-Kanazi-Kietema Km 60.65 inayotarajiwa kujengwa na Serikali kwa kiwango cha lami mkoani Kagera. |
Muonekano wa Kivuko cha Kyanyabasa kinachotoa huduma kwa wananchi wa Bukoba Vijijini ambacho kinatarajiwa kuboreshwa na Serikali ili kukidhi mahitaji ya eneo hilo. |
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa athari za mvua katika barabara hiyo Naibu Waziri Kwandikwa amesema Serikali imedhamiria kuijenga barabara hiyo kwa lami ili kukuza uchumi wa wananchi na kuwaondolea kero za mara kwa mara hasa kipindi cha mvua kubwa zinaponyesha.
"Tumejipanga kuhakikisha barabara yenu inapitika wakati wote wa mwaka hivyo kazi yenu kubwa sasa iwe kuongeza uzalishaji wa ndizi, kahawa, nyanya na miti ili mazao hayo yasafirishwe kiurahisi mijini na kukuza uchumi wa wananchi na Mkoa wa Kagera kwa ujumla," amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Amesema uchumi wa kati utafikiwa endapo maendeleo ya miundombinu yatageuzwa na wananchi kuwa fursa za uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na viwanda.
Akizungumzia kivuko cha Kyanyabasa kinachotoa huduma kwa sehemu kubwa ya wananchi wa Bukoba Vijijini, Naibu Waziri ameahidi kuwa Serikali inatafuta Kivuko kikubwa kitakachokidhi mahitaji ya wananchi ili kuchochea uzalishaji mali.
Naibu Waziri Kwandikwa yuko ziarani mkoani Kagera kukagua athari za mvua katika miundombinu ya barabara, madaraja, majengo na vivuko vinavyotoa huduma Kea wananchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment