Afisa wa Shirika la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Singida , Witness Anderson akionesha namna ya kunawa kwa usahihi kwa wananchi waliokuwa Stendi ya Mabasi ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida juzi, wakati wa kampeni ya utoaji elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona iliyofanywa na shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini Uganda kwa kushirikiana na Shirika la Stromme Foundation la Norway pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) kupitia mradi wa uwezeshaji jamii kiuchumi unaowalenga vijana.wa kiume, wa kike, watoto na wakina mama.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Amani Twaha, akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa kunawa mikono kwa wananchi wa Kata ya Chikuyu wilayani Manyoni mkoani Singida juzi.
Afisa wa Shirika SEMA, Daria John akizungumza na wananchi wa Kata ya Chikuyu kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Mwanasheria wa Shirika la SEMA, Joseph Lakati, akitoa elimu ya kujikinga na Corona kwa Mkazi wa Kata ya Chikuyu, Elizabeth Peter ambaye ni Mamalishe.
Afisa Mradi wa Shirika la SEMA, Renard Mwasambili akielekeza namna ya unawaji sahihi kwa wananchi wa Kata ya Chikuyu.
Kampeni ya utoaji elimu kwa njia ya mabango ikifanyika. Kulia ni Mary Kilimba kutoka SEMA na Kushoto ni Veronica Peter.
Afisa Mradi kutoka Shirika la SEMA, Nice Daudi, akizungumza na wananchi wa Manyoni kuhusu ugonjwa wa Corona.
Afisa wa Shirika SEMA, Veronica Peter akionesha namna ya kunawa mikono kwa usahihi kwa wakazi wa Manyoni.
Afisa wa Shirika SEMA, Gerson Janga akionesha namna ya kunawa mikono kwa usahihi kwa wakazi wa Manyoni.
Mkazi wa Manyoni, Raphael Rushu akizungumzia umuhimu wa utoaji wa elimu ya kujikinga na Corona.
Mkazi wa Manyoni, Mzee Emanuel Sajungu, akionesha namna ya kunawa mikono kwa usahihi baada ya kupata elimu.
Afisa wa Shirika SEMA, Gerson Janga (kulia) na Mary Kilimba wakitoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Manyoni.
Mkazi wa Manyoni, Sadiki Almas Nyawita akizungumzia changamoto ya wanandoa kukaribiana kama mmoja wapo atakuwa na Virusi vya ugonjwa wa Corona.
Afisa Mradi wa Shirika la SEMA, Renard Mwasambili akitoa maelekezo ya watu kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu ili kuepuka kuambukizana virusi vya corona kama itatokea mmoja kati yao atakuwa navyo.
Wafanyabiashara ndogo ndogo katika Stendi ya Mabasi ya Manyoni wakifanya biashara zao bila ya kuchukua tahadhari kusimama umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.
Kampeni ya utoaji elimu kwa njia ya mabango ikifanyika Stendi ya Mabasi ya Wilaya ya Manyoni. Kulia ni Veronica Peter kutoka SEMA na Kushoto ni Daria John.
No comments:
Post a Comment