Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (wapili kulia) akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza John Mongella na kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa
Mwanza Mhandisi Fredy Mahobe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa
mradi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani
Mwanza
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia) na wajumbe alioambatana nao
wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance
Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kuchakata
dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse akitoa taarifa ya ujenzi wa
mradi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza
mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na wajumbe
alioambatana nao katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza leo tarehe
12/05/2020.
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo na ujumbe ulioambatana naye wakiendelea na
ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu mkoani
Mwanza
Mshauri
Mwelekezi na Msimamizi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu
kinachojengwa mkoani Mwanza Libaan Yasir akionesha katika ramani namna
jengo la kiwanda cha kuchakata dhahabu kwa Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na
wajumbe walioambatana nao katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella wakihitimisha ziara ya kukagua jengo la kiwanda cha kuchakata
madini ya dhahabu mkoani.
Naibu Waziri
wa Madini, Stanslaus Nyongo kushoto akiagana na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse mara baada ya ukaguzi wa
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kuhitimishwa
Stamico ,Mkandarasi wamkosha
Naibu Waziri Nyongo
MRADI wa
ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya dhahabu nchini umeshika kasi
huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2020 na
kuifanya dhahabu ya Tanzania kusafirishwa ikiwa tayari imechakatwa na
hivyo kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la
dunia.
Ujenzi wa
kiwanda hicho ulianza rasmi mwezi Machi 2020 ambapo ujenzi wake mpaka
sasa umefikia asilimia 40, imeelezwa kuwa kukamilika kwa ujenzi wa
kiwanda hicho utapelekea suala la kisheria la kutokusafirisha madini
ghafi kutekelezwa ipasavyo.
Hayo
yamebainishwa leo tarehe 12 Mei, 2020 wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo baada ya kutembelea eneo la
ujenzi wa kiwanda hicho na taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda
hicho unaoendelea kwa kasi Mkoani Mwanza kutolewa.
Akizungumzia
mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017, Naibu Waziri Nyongo
alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutakwenda sanjari na sheria
inayowataka wafanyabiashara wa madini kutokusafirisha
madini ghafi na badala yake madini yote kusafirishwa yakiwa
yamechakatwa na kuongezewa thamani itakayopelekea kuuzwa kwa bei nzuri
katika soko la dunia.
Akizungumza
wakati wa ziara yake katika eneo hilo la ujenzi, Naibu Waziri Nyongo
alikiri kufurahishwa na usimamizi wa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) na kasi ya mkandarasi anayesimamia ujenzi wa kiwanda hicho
na kukiri kuwa Serikali itakuwa ikitembelea eneo hilo mara kwa mara
katika ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati na
kiwanda kufunguliwa kwa wakati kama
inavyotarajiwa.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameeleza kuwa
ukamilishwaji wa mradi huo utakwenda sambamba na mradi wa kuwawezesha
wachimbaji wadogo katika suala zima la kusafisha dhahabu waliyochimba
katika maeneo yao.
Aidha, Dkt.
Mwasse amesema msaada utakaotolewa kwa wachimbaji wadogo kutasaidia
kiwanda hicho kupata malighafi zakutosha kwa ajili ya kulisha kiwanda
kinachotarajiwa kuzalisha kg 480 za dhahabu kwa siku
yenye purity ya kiasi cha 999.99 ambacho ni kiwango
cha juu kabisa cha purity ya dhahabu
duniani.
Akielezea
usafi wa dhahabu itakayokuwa ikizalishwa katika kiwanda hicho, Dkt.
Mwasse amesema dhahabu hiyo itakuwa na thamani ya fedha kwa viwango
vyake na hivyo yaweza kuhifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania kama
akiba.
Aidha, Dkt.
Mwase amesema yeye na Taasisi anayoisimamia, wanajisikia fahari kubwa
kusimamia azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda na wao wakiwa
ni miongoni mwa taasisi inayosimamia viwanda mahususi kwa ajili ya
kuongeza thamani ya madini nchini na kukiri shirika la madini
linatekeleza azma hiyo kwa vitendo.
Pamoja na
hayo, Dkt. Mwasse ameahidi kusimamia kikamilifu suala la utoaji wa
kodi ya huduma pamoja na Uwajibikaji wa kiwanda hicho kwa jamii
inayozunguka mradi huo katika kutatua masuala mbalimbali ya kijamii
kama sheria inavyoelekeza.
Kwa upande
wake, Mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda hicho Libaan Yasir wa kampuni ya
Aqe Associates LTD alikiri kuwa mradi huo ulipangwa kukamilika mwezi
Desemba mwaka 2020 lakini kwa namna alivyojipanga pamoja na timu yake
watakamilisha ujenzi wa kiwanda hicho ifikapo mwezi Septemba mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment