MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiangalia mashine mbalimbali kwenye kiwanda hicho kushoto ni Mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisisitiza jambo kwa Mwekezaji wa Kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisisitiza jambo wakati
alipotembelea eneo la Kange ambako kutajengwa kitega uchumi cha Biashara
kwa Jiji la Tanga wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la
Tanga Daudi Mayeji na kulia ni Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gipson George
SERIKALI imetakiwa kuweka utaratibu utakaowezesha
taasisi za Umma na watu binafsi kuacha kuagiza kadi za kielektroniki
nje ya nchi na badala yake watumie zinazozalishwa nchini ili kujenga
uchumi wa viwanda.
Mkuu
wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella alisema hayo leo wakati
alipotembea kiwanda kipya cha kuzalisha vocha na kadi mbalimbali
kinachojulikana kwa jina Rushabh Investment Ltd kilichopo Jijini Tanga.
Alisema
akiwa kiongozi wa mkoa huo atashawishi Serikali kuweka utaratibu wa
bidhaa hizo za Kieletroniki zitakazozalishwa kiwandani hapo zitumike
katika sekta mbalimbali hapa nchini.
Shigella
alionekana kufurahishwa na uwepo wa kiwanda hicho zaidi baada ya kuelezwa kwamba kiwanda hicho pindi
kitakapoanza kazi rasmi, kitakuwa cha pili barani Afrika. Kiwanda
kingine kama hicho kipo Afrika Kusini.
"Niombe
kwa serikali mara baada ya kiwanda hiki kuanza uzalishaji basi tuachane
na uagizaji wa kadi kutoka nje ya nchini kwani sasa huduma hiyo ipo
humu nchini, na kwamba itasaidia kujenga uchumi wa nchi, " alisema
Shigella.
Mwekezaji wa
kiwanda hicho cha Rushabh Investment ltd Rashid Ahmed 'maarufu kwa jina
la Liemba' alisema uwepo wa kiwanda hicho licha ya kutoa ajira kwa
vijana hapa nchini lakini pia kitakuwa ni ukomboozi kwa nchi za Afrika.
Alisema
kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za kadi hasa katika nchi za Afrika
kutokana na kukua kwa teklonojia lakini pia nchi nyingi zinalazimika
kuagiza na kutengeneza bidhaa hizo nje ya nchi.
Hata
hivyo, Liemba ambaye ana kiwanda kingine cha kuzalisha Chokaa ya kisasa
kabisa cha Nelkant, alisema awali walikuwa wakizalisha kadi za simu
pekee lakini sasa wamekiongezea uwezo zaidi.
Alisema
wamekiendeleza ili kiweze kuzalisha kadi zote za Kieletroniki zikiwemo
kadi za benki, Bima ya afya, kadi ya mpiga kura na kadi nyingine zote,
lakini hakijaanza kazi baada ya wataalamu wake watakaoendelea na
ufungaji wa mashine kukwama nchini Ujerumani kutokana na ugonjwa wa
Covid-19.
"Kiwanda hiki
kilikuwa kianze kazi kabla ya mwezi wa nne lakini wataalamu wa mitambo
wako Ujerumanj hivyo wameshindwa kuja kufunga mitambo kutokana na
ugonjwa wa Corona.
No comments:
Post a Comment