Mtoto Samia Selemani akinawa mikono wakati wa kampeni ya utoaji elimu ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona Ilongero Wilaya ya Singida Vijijini mkoani hapa jana. Kampeni hiyo ilifanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) kwa kushirikiana na wadau kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini Uganda huku ufadhili mkuu wa mashirika hayo ukitolewa na Shirika la Stromme Foundation la Norway kupitia mradi wa uwezeshaji jamii kiuchumi unaowalenga vijana wa kiume, wa kike, watoto na wakina mama.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Amani Twaha akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Wasaidizi wa Kisheria wa Ilongero mkoani Singida ili nao wakatoe elimu hiyo kwa wananchi.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona, Amani Twaha akionesha namna sahihi ya kunawa mikono.
Msaidizi wa Kisheria, Salum Kaghondi wa Ilongero, akionesha namna ya kunawa mikono baada ya kupata elimu.
Wasaidizi wa Kisheria wa Ilongero mkoani Singida wakipata elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Kampeni ya utoaji elimu kwa njia ya mabango ikifanyika.
Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Gerson Janga akitoa elimu kwa mafundi baiskeli wa Ilongero jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa corona. .
Afisa Mtendaji wa Ilongero, Mohammed Mambo akielezea mafanikio ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Mkazi wa Ilongero, Sued Sued akizungumzia umuhimu wa Serikali kutoa idadi ya watu waliobainika kuwa na ugonjwa huo kama inavyofanywa na nchi nyingine.
Mkazi wa Ilongero, Hussein Ndeso akizungumzia ugonjwa huo ulivyobadilisha naamna ya kuswali.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa wakina mama katika Kituo cha Afya cha Ilongero.
Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo akielezea mafanikio ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa mapambano dhidi ya Corona. Kutoka kulia ni Witness Anderson, Hashim Mtahyabarwa, Muuguzi wa kituo hicho cha Afya na Ipyana Mwakyusa kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya.
Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya cha Ilongero, Grace Kishindo (kulia) , akiwaelekeza jambo wafanyakazi wenzake.
Kampeni wa njia ya mabango ikiendelea Stendi ya Mabasi ya Ilongero.
Afisa wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Daria John akitoa elimu kwa wananchi katika Stendi ya Mabasi ya Ilongero.
Afisa wa Shirika la SEMA, Veronica Peter akitoa elimu ya namna ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona wa abiria waliokuwa ndani ya Noah katika Stendi ya Mabasi ya Ilongero.
Mwanasheria wa Shirika la SEMA, Joseph Lakati, akitoa elimu kwa njia ya bango.
No comments:
Post a Comment