KWANINI WAAFRIKA WANAOMBWA KUSHIRIKI MAJARIBIO YA CHANJO? - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 19 May 2020

KWANINI WAAFRIKA WANAOMBWA KUSHIRIKI MAJARIBIO YA CHANJO?


KUMEKUWA na taarifa kadhaa za kuogofya kuhusu majaribio ya chanjo ya corona inayofanyiwa watu barani Afrika.
Hata hivyo, wanasayansi wanasema ni muhimu Waafrika washirikishwe katika majaribio ya chanjo, na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo watalemaza juhuzi za kupatikana kwa chanjo itakayofanya kazi kote ulimwenguni- na wala sio kwa nchi tajiri pekee.
Mnamo mwezi Machi, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus, alitangaza mkakati wa kimataifa wa "majaribio ya pamoja ya chanjo" kwa lengo la kutafuta dawa ya kutibu Covid-19, ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.
Kufikia sasa hakuna tiba iliyopatikana, na WHO linasema chanjo itasaidia kuzuia na kudhibiti na janga la corona.
Pia itasaidia mfumo wa kinga ya watu mwilini, kupigana na virusi na kuwazuia kuwa wagonjwa.
Kufikia sasa majaribio ya chanjo yameanza kufanya nchini Afrika Kusini - na moja inasubiri kuidhinishwa nchini Kenya. Lakini suala hilo limekumbwa na mgogoro.
Mjadala wa sasa kuhusu majaribio ya chanjo, barani Afrika umejikita katika suala la ubaguzi wa rangi.
-BBC

No comments:

Post a Comment