TANESCO NA MAPAMBANO YA VIRUSI VYA CORONA, KUHUDUMIA KWA MTANDAO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 18 April 2020

TANESCO NA MAPAMBANO YA VIRUSI VYA CORONA, KUHUDUMIA KWA MTANDAO


KUFUATIA tamko la Serikali kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya ugojwa hatari wa Corona (Covid-19),

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwafahamisha wateja wote na wananchi kwa ujumla, kuwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona, TANESCO itaendelea kufuata taratibu zote za kuchukua thadari zinazotolewa   na Wizara ya Afya kwa kupunguza msongamano wa watu usio wa lazma katika ofisi zote za Shirika ili kuweza kuwakinga watumishi na maambukizi ya Corona.  

Ili kufanikisha maelekezo haya ya Serikali kwa ufanisi mkubwa TANESCO inawashauri wateja wetu katika kipindi hiki.

Kutumia njia zetu mbadala za mawasiliano ikiwa ni pamoja na simu au barua pepe pamoja na mitandao ya kijamii na ‘‘TANESCO app’’, ili kufikisha matatizo maoni na maombi ya wateja kwa Shirika, na changamoto zozote za huduma wanazo pata ili zipatiwe utatuzi kwa wakati, hii itasaidia kupunguza msongamano wa wateja katika ofisi zetu.

Kuanzia Jumatatu tarehe April 20, 2020  Wateja   na Wageni wote watakaofika katika Ofisi za shirika watalazimika kuvaa Barakoa (face mask) ndipo wapate ruhusa ya kuingia katika  Ofisi za Shirika , pia kuzingatia taratibu zote za kiusalama zilizowekwa katika ofisi zetu ikiwemo kunawa mikono kwa kutumia vitakasa mikono (sanitizers) vilivyowekwa katika kila ofisi, kabla ya kuingia katika ofisi husika na wakati wa kutoka.

TANESCO itaendelea kuchukua hatua zote muhimu za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona bila kuathiri utendaji wa kazi za Shirika  na utoaji huduma kwa wateja wetu.

TANESCO inawashukuru kwa ushirikiano wenu.


Imetolewa na:  Ofisi ya Uhusiano
                        TANESCO-Makao Makuu
                         DODOMA

No comments:

Post a Comment