Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa kulia akizungumza wakati akishukuru Taasisi ya Odo Ummy
Foundation kwa msaada ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya
kuwekea
ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na
maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia katikati
ni Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga.
Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy
Foundation Khatibu Kilenga kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa kushoto kabla ya kuona msaada
ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea
ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na
maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia ambayo
vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa nyumba za ibada
misikiti na makanisa Jijini Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa kushoto akiangalia koki zilizopo kwenye ndoo hizo ambazo
zilitolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa
kwenye misikiti na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa
wa Corona.
Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa na
Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa kwenye misikiti
na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona.
Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa kwenye misikiti na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona. |
NA MWANDISHI WETU, TANGA
TAASISI ya Odo Ummy Foundation ya Jijini Tanga imetoa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa taasisi za dini zilizopo Jijini humu ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanaepukana na maambukizi hayo kwa kuchukua tahadhari.
Msaada uliotolewa ni ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisa dunia.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa, Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation, Khatibu Kilenga ambayo ilianzishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Ummy Mwalimu ikiwa na lengo la kujenga hamasa kwenye jamii na kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii.
Alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikiwasaidia kwenye mambo mengi ikiwemo elimu, afya na makundi madogo madogo ya kijamii ikiwemo vijana na wanawake ili kuweza kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kupitia fursa zilizopo kwenye maeneo yao na hivyo kuharakisha maendeleo.
“Kwenye janga hilo lililoikumba dunia la Corona hatukuwa nyuma tumeona angalu tutoa ndoo na sabuni kwa ajili ya kusaidia kupunguza maambukizi ambao yanaonekana kukua kwa kasi kwenye maeneo mbalimbali lakini pia ni sehemu ya kutoa elimu pamoja na kwamba kuna maelekezo mbalimbali yanayotolewa ya kujilinda kwa kunawa mikono vizuri pamoja na kutumia maski, ”alisema.
Aidha alisema wao wameona wagawe ndoo 60 maana ya zenye maji na za kukingilizia 60 hivyo kufikia ndoo 120 na vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ambayo watazigawa kwenye maeneo ya misikitini na kanisani ambapo wameona kutakuwa na uhaba mkubwa.
“Katika maeneo ya ibada misikitini na kanisani tuliona vifaa hivyo havijawafikia na ndio maana tuliona tusambaze huku akisisitiza kwamba hiyo ni hatua ya kwanza ya kusaidia jambo hilo lakini hapo mbeleni wanakusudia kufanya jambo mkubwa zaidi”Alisema Kilenga.
Hata hivyo alisema pia wataendelea kuchangia mambo mbalimbali kwa jamii kwani matatizo yao ni yetu na hivyo ndio kauli mbiu ya Taasisi yetu kwamba “Tanga yetu ni wajibu wetu” huku akimkaribisha Mkuu huyo wa wilaya ashiriki nao katika kuliunga mkono jambo hilo akiwa kama msimamikzi mkuu wa wilaya.
Awali akizungumza wakati wa alipotembelea na kuona vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliishukuru Taasisi ya Oddo Ummy Foundation na Mbunge Ummy kwa kuja na mpango huo wa kusaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka ambapo kwa sasa wamekuwa wakikabiliana na ugonjwa wa Corona.
Alisema ni faraja kubwa kwa kuja na mpango huo wa kutusaidia watu wa Tanga vifaa hivyo kufanyia jambo la usafi ambalo ni sharti la umuhimu katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
“Lakini nishukuru Taasisi ya Oddo Ummy foundation kuianisha msaada huo ujieleze kwenye maeneo gani hilo ni jambo la msingi sana na muhimu hivyo tunakushukuru sana kwa hili ambalo umelifanya kupitia Taasisi yenu na tunafurahi kuona umeelekeza hili liende kwenye jumba za ibada,”alisema.
Aidha alisema kwamba wamefurahi sana kuona msaada huo uelekezwe kwenye nyumba za ibada na itakuwa ni mchango mkubwa sana kwao kuweza kuimarisha jitihada mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ambao ni hatari duniani.
“Msaada huo umekuja kutupa nguvu kwa juhudi ambazo tumekuwa tukizifanya hivyo tunakushukuru sana huku akizitaka taasisi za dini ambazo zitanufaika na msaada huo kuhakikisha wanavitumia kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo."Alisema DC Mwilapwa.
No comments:
Post a Comment