Waziri
wa nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Iringa katika bwawa la Mtera akitoa katazo la kuwepo kwa mgao wa umeme hapa nchini.
Waziri
wa nishati Dkt Medard Kalemani akiwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipofanya ziara katika bwawa la Mtera.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WAZIRI wa nishati Dkt Medard Kalemani amepiga marufuku kwa
uongozi wa TANESCO kutoa nishati ya umeme kwa mgao wakati hakuna tatizo lolote
la uzalishaji katika vituo vyote vitatu.
Akizungumza
wakati wa ziara katika kituo cha uzalisha ji wa umeme Mtera mkoani iringa,Dkt Medard Kalemani alisema kuwa “haiwezekani mtu mmoja anaamua kutoa maagizo ya kuwepo
mgao wakati hakuna tatizo lolote lile”.
Alitoa
agizo hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
Mhandisi Felchesmi Mramba Kuhakikisha anamchukulia hatua mfanyakazi aitwae
Abubakari kwa kosa la kuagiza mkoa wa Mwanza kuwepo kwa mgao wa umeme bila
sababu za msingi.
"Usipomchukulia
hatua huyu mfanyakazi anaeitwa Abubakari basi Mimi nitajua nani wa kumchukulia
hatua kwa kuwa tatizo hilo kwa Abubakari limekuwa likijirudia mara kwa mara"
alisema
Alisema
serikali imejenga nyumba za wafanyazi pale ubongo kwa ajili ya uangaliangalizi
wa mwenendo wa umeme nchi nzima lakini bado wafanyakazi wanakaidi kukaa hapo jambo
linalopelekea ufanisi wa kazi kuwa hafifu.
Aliwaagiza
Mameneja wa TANESCO mikoa yote hapa nchini kuhakikisha wanawasimamia vilivyo
wafanyakazi wengine ili watimize wajibu wao katika kutimiza ahadi ya kutoa
huduma ya nishati kwa wananchi.
Aidha
Dkt. Medard Kalemani alitoa tahadhari kwa wananchi
waliokaribu na mto Ruaha mkuu kuchukua tahadhari kwa kuwa wameamua kufungulia
maji kutoka katika bwawa la Mtera na Kidatu kutokana na kujaa hadi kupitiliza
kiwango kinacho hitajika.
Alisema
Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari na kuongeza kuwa maji hayatakuwa
yanasambaa bali yatapita kwenye mkondo wake wa asili ambako wananchi wanafanya
shughuli zao za kijamii.
"TANESCO
tumeona ni muhimu kutoa tahadhari kwa Wananchi kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha, kwa kawaida Bwawa la Mtera kulijaza huchukua miezi 3 hadi 4 kwa mvua
za masika, lakini kwa kipindi hiki mvua za vuli zimekuwa nyingi ndani ya mwezi
mmoja hivyo kina kimeongezeka", alisema
Alisema
tahadhari inatolewa kwa Wananchi kusitisha shughuli zao za kijamii kama uvuvi,
kulisha mifugo, kilimo na nyingine kwenye mkondo wa maji au sehemu zenye
vidimbwi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Aliongeza
kuwa, kawaida kina cha maji kujaa ni mita 698.50 juu ya usawa bahari na
kuongeza hivi sasa kina cha maji kimefikia 698.03 juu ya usawa wa bahari.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa wamekuwa
wakitoa elimu mara kwa mara kwa wananchi kwa lengo la kuwaokoa wananchi na
madhara ambayo wanaweza kuyapata kipindiki cha mafuriko hasa wale wanaofanya
shughuli katika bwawa la Mtera na kandokando ya mto Ruaha.
Kasesela
alisema kuwa historia inaonyesha kila baada ya miaka kumi mvua hunyesha kwa
wingi kama ilivyo hivi sasa na kupelekea bwawa hilo la Mtera kujaza maji kupita
kiasi hivyo lazima kuwepo kwa mkakati maalumu wa kila mwaka kutoa elimu kwa
wananchi.
“Hii
ni historia ambayo nimeikuta na nimeona ikifanya kazi kama hivi ambavyo tunaona
bwawa limejaa maji hadi kupita vipimo vinavyotakiwa kwenye bwawa hili” alisema
Kasesela
Kasesela
alimuomba waziri kusaidia kuharakisha ujenzi wa daraja jipya ambalo michoro
yote imekamilika ila fedha bado hazijapatika kwa lengo la kuliokoa daraja la
sasa kutokana na magari yanayopita hapo yanauzito mkubwa sana
No comments:
Post a Comment