DC KASESELA:AHAMISHA KITONGOJI CHA MBINGAMA TARAFA YA PAWAGA. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 23 March 2020

DC KASESELA:AHAMISHA KITONGOJI CHA MBINGAMA TARAFA YA PAWAGA.

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wananchi wa kijiji cha Isele kitongoji cha Mbingama kilichopo katika tarafa ya Pawaga akiongea nao mara baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na kunyesha kwa mvua nyingi mwaka huu.

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wananchi wa kijiji cha Isele kitongoji cha Mbingama kilichopo katika tarafa ya Pawaga akiongea nao mara baada ya kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na kunyesha kwa mvua nyingi mwaka huu.


NA FREDY MGUNDA,PAWAGA IRINGA.

WANANCHI wa kitongoji cha Mbingama Kijiji cha Isele wilaya ya Iringa mkoani Iringa wametakiwa kuhama moja kwa moja ili kuepukana na mafuriko ambayo yamekuwa yanasababisha anguko la kiuchumi,afya na maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kuwatembelea wahanga wa mafiriko katika tarafa ya pawaga,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipiga marufuku wananchi kurudi kuishi katika kitongoji hicho.

Alisema kuwa ili kuepukana na mafuriko ya kila mwaka lazima wananchi wahame katika kitongoji hicho ambacho kimekuwa kikipata mafuriko ya mara kwa Mara.

Mwaka 2016 kitongoji cha kilala ambacho kwa sasa kinaitwa Kasesela kilikumbwa na mafuriko makubwa lakini baada ya kuwahamisha wananchi kutoka kule na kwenda eneo jingine hakuna  tena mafuriko

"Napiga marufuku wananchi yeyeto kurudi kuishi kule ambako mafuriko yametokea ili kuepukana tena na tatizo la janga hili la mafuriko" alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wataalamu wa sekta ya maji,afya,ardhi na miundombinu kuhakikisha kuanzia kesho wanahamia katika eneo la mafuriko ili kutatua changamoto ambazo waathirika wa mafuriko wanakumbana nazo.

Awali akimueleza mkuu wa wilaya,mwenyekiti wa kijiji cha Isele Ballo Halfani alisema kuwa wananchi wamepoteza Mali nyingi hivyo kuna njaa,hakuna sehemu ya kulala, maswala ya afya na hakuna hata mbegu za kulimia.

Halfani alisema kuwa wananchi takribani mia nane na moja na kaya 218 ndio waathirika wa mafuriko katika kitongoji cha mbingama.
Akizungumza kwa niamba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa,afisa elimu msingi Peter Fusi alisema kuwa serikali imeleta chakula na itaendelea kusaidia wahanga wote hadi pale janga hilo litakapoisha.

Fusi aliwasihii wananchi kuhakikisha  wanajikinga na magonjwa ya mlipuko na corona katika kitongoji hicho hivyo wanatakiwa kujua tahadhari ya kujikinga na magonjwa hayo.

No comments:

Post a Comment